Mashabiki Wanaweza Kuwa Mapato Kwa Klabu

Klabu kubwa nyingi duniani zimekuwa zikitumia mashabiki kama sehemu ya kujipatia mapato ili kuendesha shughuli mbalimbali za klabu ikiwemo usajili, mishahara na hata matumizi mengine ya klabu.

Maendeleo haya makubwa yanaonekana huko mambele yaani bara la Ulaya na baadhi ya klabu zilizo ukanda wa Afrika kaskazini. Tanzania bado sana kwa klabu kutumia fans wao ili kujiweka vyema kwenye masuala ya mapato toka kwa mashabiki.

Timu nyingi za Tanzania zinakuwa na kadi za wanachama ambazo zinalipiwa kwa mwaka, na wanachama wenyewe aghalabu huwa ni wazee na hawa hawa ndio ambao wanahudhuria vikao. Hali ya kuwa kuna vijana wengi sana ambao ni mashabiki!

Mchambuzi wa soka FarhanJr, anaamini kuwa klabu za Tanzania zinaweza kujitengenezea muhimili mkubwa sana wa mapato kutoka kwa fans  wao endapo wataanza mazingira mazuri ya kuwageuza mashabiki vijana kwenda kwenye kuwa wa kudumu.

Simba
moja ya shabiki wa Simba akiwa anafurahia kuona kikosi cha Simba

Klabu za Simba na Yanga za Tanzania zina wadau wengi sana ambao wamekuwa wakionekana kuzaliwa na mahaba ya kuchagua moja ya hizi klabu kubwa toka utotoni kabisa, endapo klabu hizi zitaandaa mashabiki watakaoweza kuwa wanachama baadae basi watakuwa wameshinda sana kujipatia mapato.

Mashabiki
Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao

Katika mkutano wa Yanga hapo jana, kulikuwa na mapato kidogo sana yaliyotoka kwa wadau lakini Yanga hii ina wapenzi wakereketwa wengi sana ambao kama ingeamua kuwatengenezea mazingira basi ingekusanya mkwanja mrefu sana! na Inawezekana!


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

United, United Wakutana na Mawakala wa Camavinga, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe