Nahodha wa timu ya taifa ya Senegal Kalidou Koulibaly amesema kutokuwepo kwa Mane kwenye timu ya taifa sio tatizo kwani bado staa huyo anawapa nguvu wachezaji wenzake.

Saido Mane ambaye alipata majeraha katika mchezo wa Bundesliga ambapo alikua akiitumikia klabu yake ya Bayern Munich na kumsabisha kukosa fainali za kombe la dunia nchini Qatar.koulibalyKoulibaly amesema licha Mane kukukosekana katika kikosi hicho bado mtoa hamasa mkubwa na nguvu kwenye timu hiyo kutokana na ukaribu ambao amekua anao na kambi ya timu ya taifa ya Senegal wakati huu michuano ikiendelea nchini Qatar.

Senegal ambao walipoteza mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi kwa mabao mawili kwa bila wanajiandaa kutupa karata yao katika mchezo wa pili watakaomenyana na wenyeji timu ya taifa ya Qatar ili kutetea nafasi yao ya kubaki michuanoni.koulibalyKolibaly aliendelea kusisitiza umuhimu wa Mne kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Senegal na kueleza wanajua umuhimu wake hivo wanaamini ataendlea kujumuika nao kwa karibu ili kuendelea kuwapa nguvu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa