Timu ya taifa ya Cameroon imeanza vibaya katika michuano ya kombe la dunia baada ya kukubali kipigo cha bao moja kwa sifuri dhidi ya timu ya taifa ya Uswisi katika mchezo uliopigwa mapema leo saa saba mchana.

Imekua mwendelezo wa timu za Afrika kuendelea kusuasua kwenye michuano hiyo baada ya timu nne kutoka Afrika kujitupa uwanjani mpaka sasa huku timu mbili zikiwa zimefungwa huku huku mbili zikiwa zimepata sare.cameroonCameroon chini ya kocha mzawa Rigobert Song ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo wameshindwa kuanza vizuri kwenye michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha bao moja kwa bila licha kuonesha ushindani mkubwa katika mchezo huo.

Bao pekee la Breel Embolo lilitosha kuwazamisha Simba wasiofugika na kuwapa alama tatu muhimu timu ya taifa ya Uswisi huku wakiwapa mtihani mzito vijana wa Song kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika michezo inayofuata.cameroonHabari kubwa katika mchezo huo ilikua ni mfungaji wa bao Breel Embolo ambaye baada ya kufunga bao katika mchezo huo hakushangilia kwakua ameifunga timu ya taifa lake alipozaliwa. Embolo yeye alizaliwa katika mji wa Younde nchini Cameroon mwaka 1997.

machaguo spesho

Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa