Upasuaji wa beki  Yasser Al Shahrani wa timu ya taifa ya Saudia Arabia umefanikiwa salama siku ya leo taarifa rasmi kutoka kambi ya timu hiyo imesema.

Beki huyo ambaye aligongana na golikipa wake katika mchezo wao dhidi ya timu ya taifa ya Argentina ambapo walipata ushindi na kumfanya beki huyo kupasuka kichwani na kufanyiwa upasuaji ambao umefanikiwa leo hii.saudia arabiaKupitia ukrasa rasmi wa mtandao wa Twitter wa timu ya taifa ya Saudia Arabia umeeleza kua upasuaji wa Al Shahrani umekamilika salama leo lakini taarifa beki huyo kama ataendelea kushiriki michuano hiyo bado zikiwa hazijawekwa wazi na timu hiyo.

Saudia Arabia ambao wanajiandaa kucheza na timu ya taifa ya Poland katika mchezo unaofuata baada ya kupata ushindi katika mechi ya kwanza dhidi ya vigogo Argentina. Mchezo dhidi ya Poland utatoa taswira ya kusonga mbele kwa timu hiyo endapo watashinda mchezo huo.saudia arabiaKikosi hicho kinachonnolewa na mwalimu Herve Renard amabe amewahi kuchukua ubingwa wa Afrika na timu ya taifa ya Zambia mwaka 2012,imewashtua watu wengi baada ya kupata matokeo dhidi ya Argentina na kuwafanya kua timu ya kutupiwa macho kwenye michuano hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa