Mason Mount: Tutarudi Tukiwa Imara Zaidi

Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza anayekipiga katika klabu ya Chelsea Mason Mount amesema anaamini watazinduka na kurudi wakiwa imara zaidi baada ya kupata huzuni ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la dunia katika hatua ya robo fainali.

Kiungo aliinuliwa katika benchi na kuingia katika mchezo ambao walitolewa na timu ya taifa ya Ufaransa kwa mabao mawili kwa moja, Mount ambaye alipoingia tu alikwenda kusababisha mkwaju wa penati baada ya kuchezewa faulo kwenye eneo la hatari.mason mountKiungo huyo baada ya kuingia alileta mabadiliko chanya baada ya kusababisha penati ambayo nanhodha wa timu hiyo kama angepata basi ingeufanya mchezo kuanza upya. Kane alikosa penati pale ambapo walikua nyuma kwa mabao mawili kwa moja.

Mason Mount anasema licha ya kuelewa itachukua muda mpaka maumivu hayo kukatika lakini anaamini watazinduka kwenye maumivu hayo na kurudi imara zaidi ili kuendelea kuipeperusha bendera ya timu ya taifa ya Uingereza kweye michuano mbalimbali.mason mountTimu ya taifa ya Uingereza kwa mwaka huu imeporomoka kwenye michuano ya kombe la dunia kwani michuano iliyomalizika walifanikiwa kufika hatua ya nusu fainali, Lakini mwaka huu wametolewa kwenye hatua ya robo fainali na mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya taifa ya Ufaransa.

Acha ujumbe