Kocha mkuu wa Brentford Thomas Frank amesema kuwa anaamini kuwa mchezaji wake Ivan Toney anaweza kuwathibitishia watu kuwa wanakosea baada ya kushindwa kuingia uwanjani katika mojawapo ya Ligi ya Mataifa ya England wakati wa mapumziko ya Kimataifa.
Ambapo mchezaji huyo aliachwa nje ya kikosi cha siku ya mechi Gareth Southgate kwa kichapo cha 1-0 kutoka kwa Italia na wakati wakati huo huo alijumuishwa katika wachezaji 23 waliochaguliwa kwa mechi ya Ujerumani hakuitwa nje ya benchi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alikuwa ameitwa kwa mara ya kwanza na Southgate baada ya kuanza vyema msimu huu ambapo alifunga mara tano katika mechi sita za kwanza za ligi ya Brentford.
Na Frank anasema Toney lazima atumie hali hii ya kukatishwa tamaa ili kuongeza ubora wake kwenye kikosi cha Brentford, akiwaambia waandishi wa habari: “Bila shaka Ivan alitarajia kuingia uwanjani”.
Frank anasema anadhani katika maisha na soka jinsi unavyopata mafanikio unaweza kuonyesha uthabiti na kurudi kutoka kwa vikwazo vidogo. Mchezaji unatakiwa urudi nyuma kidogo, usikate tamaa lakini unahitaji kusonga mbele na kuthibitisha kwa watu makosa kwa kufanya vizuri na ndicho kitu pekee cha kufanya.
“Kwa hivyo ni rahisi kiasi. Lakini ni vigumu zaidi kuifanya siku baada ya siku. Lakini Ivan ana mawazo madhubuti na atafanya kila awezalo kufanya vyema.”