Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Colombia na Real Madrid Freddy Rincon amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 55 huko Cali, Colombia.

Siku ya Jumatatu ripoti zilieleza kuwa Rincon alihusika katika ajali ya gari kati ya gari lake na basi. Alipelekwa hospitali na kulazwa katika chumba cha upasuaji wa dharura.

Baada ya kutumia siku tatu kupigania maisha yake katika chumba cha wagonjwa mahututi, Rincon aliaga dunia Jumatano usiku saa za huko. Alikuwa amefanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo katika jaribio la kuokoa maisha yake.

Wengine pia walijeruhiwa katika ajali hiyo lakini wanaonekana kuwa katika hali nzuri.

Freddy Rincon
Freddy Rincon

Rincon alicheza soka la kulipwa kwa jumla ya miaka 18 huko Brazil, Colombia, Italia na Uhispania, pamoja na Real Madrid. Aliichezea Colombia mechi 84 na alicheza katika Fainali za Kombe la Dunia mara tatu mfululizo mwaka wa 1990, 1994 na 1998. Shirikisho la Soka la Colombia lilikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuomboleza kifo chake.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa