Furaha Yenye Karaha!

Mchezaji huwa huru kuzitumia hisia zake kushangilia vile anavyojisikia yeye kwa namna ambayo itaheshimu nafasi ya wengine bila kuhatarisha au kuvunja sheria ambazo zimewekwa kama zile zinazoonesha kushangilia kwa kuashiria kitu fulani au kumfanya mwingine akose amani kwa sababu ya hilo.

Pia, kuna msemo usemao, “Furaha ikizidi hugeuka kilio”. Hili limetokea pale Ronaldo alipowafunga Atletico magoli matatu kitu ambacho alishindwa kujizuia kutokana na kujenga historia ya kuipeleka klabu yake kwenye hatua ya robo fainali baada ya kusawazisha idadi ya magoli ambayo awali walifungwa na kugeuza kabisa matokeo ndani ya mechi ile.

Baada ya kufikia idadi ya magoli hayo matatu aliweza kushangilia kwa kujibu mapigo yaliyofanywa na Simeone, kocha huyo aliweza kushangilia kumuonesha Ronaldo kwamba hawana namna wanaweza kuwashusha wao akiwa ndani ya klabu yake hiyo mpya lakini Ronaldo baada ya kurudisha magoli hayo kwa historia ya ajabu alishangilia jambo lililomfanya achunguzwe.

Baada ya penati yake zikiwa zimesalia dakika nne tu kukamilika kwa dakika za mchezo huo, aliweza kuzamisha mpira wake huo nyavuni na kuandika bao lake la tatu ikiwa ni katika dakika za mwisho kabisa za mchezo huo baina ya miamba hao. Kupitia goli lake akafanikisha kuipeleka timu yake kwenye hatua inayofuata.

Goli lake ambalo lilitengeneza matokeo ya 3-2 baada ya kufuta makosa yao ya 2-0. Kupitia aina yake ya ushangiliaji, Ronaldo alionesha vitendo vya matusi pale aliposhika nyeti zake na kuanza kuwapigia mashabiki wa klabu hiyo na uongozi wao huku akijua kabisa mazingira ya akifanyacho sio mazuri.

Hadi sasa maamzi ya adhabu hiyo atakayokutana nayo mchezaji huyo ni katika kukemea ulipaji wa visasi kwenye jambo fulani pia kuharibu kabisa nguvu za kishetani zinazovuruga amani ya wengine. Na maamzi ya hilo yatatolewa siku ya tarehe 21. Kocha wa klabu hiyo ana amani kabisa kwamba mchezaji wake hawezi kukumbwa na adhabu au faini yoyote.

Kwa hatua hiyo, Juventus baada ya kufuzu katika hatua hiyo watakutana na Ajax kwenye mechi inayotegemewa kuwa ngumu na yenye kuvutia itakayochezwa tarehe 10, Aprili kule Amsterdam na kurudiwa tarehe 16, Aprili kule Turin ambapo kila mmoja kwa nafasi yake atatumia uwanja wa nyumbani kwa namna atavyoweza kutafuta ushindi.

Ikumbukwe kwamba Simeone alipigwa faini ya kiasi cha $22,000 kwa kosa linaloendana na hilo hivyo kuna uwezekano mkubwa hata Ronaldo asiweze kukwepa suala hilo. Katika suala la takwimu Ronaldo ndiye mfungaji wa kihistoria akiwa na magoli 124 katika mechi 160 alizocheza tayari.

3 Komentara

    Habari nzuri

    Jibu

    Iko poa.

    Jibu

    Gud newa

    Jibu

Acha ujumbe