Mshambualiaji wa Manchester United, Alexis Sanchez ameamua kufunguka kwa wale wanaomdhania mabaya kwamba angeweza kuondoka katika ardhi ya Uingereza na kujiunga na klabu nyingine kutokana na kukosa muda wa kutosha wa kuonesha makali yake ndani ya uwanja kitu ambacho kwake hakipi nafasi kabisa na hakisumbui akili yake.
Alichokitolea maelezo ni kwamba kwa sasa anaangalia namna atakavyopigana kuhakikisha anawapa vikombe United na anafurahia maisha ya klabuni hapo na yupo tayari kukomaa na maisha ya hapo kwa kujitoa kwa nguvu zake zote kuhakikisha anarudisha heshima hiyo, pia anataka kurudi kwenye kiwango chake kama ilivyokuwa katika kikosi chake cha Chile.
Sanchez, ambaye kwa sasa hayupo katika kikosi cha United kutokana na majeraha yake aliyoyapata wakati wa mechi dhidi ya Southampton, amecheza mechi 23 pekee kwa msimu huu akiwa amefanikiwa kufunga magoli mawili na kutoa pasi nne za magoli kitu kinachofanya aendelee kuhangaika kurejea kwenye ubora wake wa awali.

Japo uongozi wa klabu hiyo bado unampa nafasi ya kufanya vyema mchezaji huyo na una imani ataweza kufanya makubwa na klabu hiyo wanaweza kumpa muda zaidi kuona kama anaweza kurejesha uimara wake ndani ya kikosi chao ikiwa ni katika kufunga na kurejesha furaha ya mashabiki ambao wanaamini makubwa sana kutoka kwake.
Kikubwa kwake kwa sasa ni kuhakikisha mashabiki waliokuwa na imani kubwa kwake wanapata madini yote na kufurahia usajili wake na mshahara anaolipwa kikosini hapo kwani ni haki yao kuhakikisha mchezaji anaiwakilisha vyema klabu yake kwenye michuano yote mikubwa ambayo klabu hiyo inashiriki. Kwa kufanya hilo atakuwa amefanikiwa kuwakamata mashabiki hao.
Sanchez ameenda mbali sana kwa kukumbusha siku walipopoteza mechi yao ya FA mbele ya Chelsea katika uwanja wa Wembley, anasema alihuzunika sana na kujiona kama wameshusha kabisa imani ya mashabiki ambao kwake walimpa ile furaha kubwa kutokana na muonekano wao ambapo walikuwa kwenye vazi linalowafanya wapendezeshe uwanja kama mashabiki wa United kweli; kitu hicho kilimpa imani kubwa.
Mchezaji huyo amefunguka pia suala zima la maisha yake ndani ya Chile ya kwamba taifa lake hilo ni dogo sana lakini ni taifa ambalo linampa furaha kubwa sana na anajisifia sana kuwa ndani ya taifa hilo na anachokiangalia zaidi ni kitu gani anachokipenda sana kwenye maisha yake ya soka. Amefunguka wazi kwamba anapenda sana soka kama kitu chake cha kwanza kabisa na kingine ni mapenzi na wanyama wanaofungwa nyumbani.
Kitu cha kuamini kwa mchezaji huyo ni kwamba ana uwezo mkubwa na ni imani ya kila mmoja kwamba katika umri wake wa miaka 30 bado ana nafasi kubwa ya kufanya mengi zaidi na kikosi hicho kwa sababu historia yake ni pana na sio mchezaji anayebahatisha.


isha
Ahsante kwa kutuelekeza
Lydia Emmanuel Magoti
Safii Sana kwakutujulisha
Furahav
Safi
Issa
Sanchez bonge la mchezaji