Crystal Palace wamewasilisha ombi la takriban paundi milioni 27 juu ya mchezaji Conor Gallagher baada ya kuongeza juhudi za kumnunua tena kiungo huyo kutoka Chelsea, kwa mujibu wa The Times.

Palace wana matumaini kuwa, wanaweza kumshawishi Gallagher na Chelsea kukubali uhamisho wa kudumu badala ya yeye kuhama kwa msimu wa pili mfululizo kwa mkopo.

Gallagher Ahitajika na Crystal Palace
Kiungo wa Chelsea-Conor Gallagher

Kiungo huyo ameanza mechi mbili zilizopita za Chelsea na kuomba msamaha kwa wachezaji wenzake na wafuasi wa klabu hiyo baada ya kutolewa nje kwa kadi mbili za njano ndani ya dakika 28 za ushindi wa 2-1 dhidi ya Leicester City Jumamosi. Kiungo huyo amekuwa Chelsea tangu akiwa na umri wa miaka minane na ana mkataba hadi mwaka 2025.

Gallagher Ahitajika na Crystal Palace

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa