Gerard Pique baada ya kuvuja kwa maongezi yake na rais wa shirikisho la mpira nchini Hispania kuhusu ushawishi wake wa kutaka michuano hiyo kuamishwa kwenda mashariki ya kati kuna audio nyingine imetoka ambayo anasikika akitumia jina la Leo Messi kwenye ushawishi wake.
Kwenye mazungumzo ya mlinzi huyi wa kati wa klabu ya Barcelona na rais wa RFEF Luis Rubiales yamesababisha kutokea kwa sintofahamu, El Confidencial wakivujisha jumbe za sauti kuhusu uhamisho wa mashindano ya Supercopa de Espana.
Gerard Pique ndio mtu muhimu kwenye uhamisho wa mashindano kutoka kuchezwa kwenye michezo ya kujiandaa na msimu hadi majira ya baridi na kutoka Hispania hadi Morroco na kisha Saudi Arabia.
Kilachoshangaza ni kutumika kwa mchezaji bora wa dunia kwenye ushawishi huo wa kuhamisha mashindano hayo, Kulingana Diario Sport amabao wanadai kuwa Gerard Pique alitumia wazo la kumtumia messi ili kufanikisha mpango huo.
” Pia tunae Messi nyuma yetu, atatumia video na kila kitu, kwaiyo tunaweza kusema kwamba ujumbe huu wote ni kutoka kapteni wa Barcelona.” alisema Pique.
Ambapo Rubiales alijibu,” vizuri, sharti kidogo. Usiweke sharti hili, lakini waambie kwamba utawatumia video yako na pia messi kama hivyo.”
Kulingana na chanzo cha habari cha Diario Sport, kimeweka wazi kuwa Messi hakuweza kurekodi video na hakukubali ombi la Pique.
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.