Winga wa Bercelona, Ousmane Dembele amethibitisha kuwa hakuna taarifa yeyote ya ziada juu ya mazungumzo ya kukubaliana mkataba mpya na Barcelona.
Ronald Koeman amekuwa akisisitiza nia yake ya kutaka kumbakiza nyota huyu wa Ufaransa pale Camp Nou wakati mkataba wake wa sasa ukiwa unafika mwisho mwisho wa msimu ujao.
Hata hivyo, hakujawa na maendeleo yeyote kwenye mazungumzo ya mkataba mpya, kwa mujibu wa Dembele kama alivyonukuliwa na Marca. Licha ya kuwepo na hali hii Dembele bado ana matumaini kuwa hatma yake klabuni hapo itapewa umuhimu.
“Hakuna mazungumzo yeyote bado juu ya mkataba mpya, lakini najihisi vyema tu” – Ousmane Dembele

Nyota huyu wa zamani wa Borussia Dortmund anafurahia msimu wake bomba akiwa na Barcelona, akiwa sehemu ya ushambuliaji pamoja na Lionel Messi, Antoine Griezmann.
Nyota huyu wa miaka 23 amebainisha kuwa kwa mwaka 2021 amefurahia zaidi kucheza kama mshambuliaji, na amecheza jumla ya mechi 24 za ligi kwa msimu huu wa 2020-21.
Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.



dorophina
Dembele ni bora abakie camp nou
Sarah
Dembele yuko vizuri
Venerose
Dembele yuko vinzur
Hopemwaikuka
Eeh
warda
Hawawezi muuza mpaka wapate mbadala