Okwi Kurejea Simba?

Inasemekana kuwa nyota wa zamani wa kikosi cha Simba, Emanuel Okwi yupo kwenye hesabu za kurejea ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Dider Gomes.

Wakati kikosi cha Simba kilipotua nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, aliwatembelea kambiniAprili 9 na kuzungumza na wachezaji wa Simba.

Okwi

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Al Salaam Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kuwafanya waache pointi tatu mazima nchini Cairo ikiwa ni mchezo wao wa kwanza kupoteza hatua ya makundi baada ya kucheza mechi tano bila kufungwa.

Kwa sasa Okwi anacheza nchini Misri soka la kulipwa katika Klabu ya Ittihad ambapo msimu huu 2020/21 amecheza mechi 9 na kutumia dakika 493 na ametupia mabao mawili.

Okwi
Klabu ya Ittihad

Alijiunga na timu hiyo msimu wa 2019/20 baada ya mkataba wake na Simba kuisha na kulikuwa na mvutano mkubwa kwenye upande wa kuongeza mkataba wake.

Ndani ya timu yake ya sasa nchini Misri mkataba wake unamalizika msimu huu jambo ambalo linaongeza nafasi ya Simba kumtwaa mchezaji huyo bure.

Okwi

Kuhusu suala hilo Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema:“Usiniulize kama Okwi ambae kwa sasa anacheza soka la kulipwa Misri atarejea kucheza Simba au laa msimu ujao ila jua kwamba mkataba wake na timu yake upo ukingoni,”.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

5 Komentara

    Okwi akirejea simba itakuwa poa sana

    Jibu

    Itakuwa poa sana

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Cjapenda

    Jibu

    Itakuwa poa sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.