Mkurugenzi wa zamani wa Inter Milan, Marco Branca amesema kuwa hatma ya meneja Antonio Conte pale Inter inategemea na namna atakavyowashawishi wamiliki wa klabu hiyo.
Inter wanaendelea kuongoza msimamo wa Ligi kwa tofauti ya pointi 11 dhidi ya AC Milan ambao wapo nafasi ya pili. Inter wanahitaji pointi 13 zaidi kushinda taji la Serie A kwa mara ya kwanza baada ya kusubiri kwa zaidi ya miaka 10.
Mkataba wa sasa wa Antonio Conte unaisha 2022, lakini Branca bado hana uhakika kama meneja huyu ataendelea kuwapo Inter.

Katika mengi aliyozungumza na kituo cha redio cha Punto Nuovo, alisema;
“Unatakiwa kujua Sunnings wana mipango gani kwanza. Kisha bodi itaamua na kuona namna gani ya kusonga mbele kwenye michuano Ulaya. Vivyo hivyo kwa Milan, wale wanaotazama talanta za vijana.”
“Inter ni timu pekee iliyocheza kwa kiwango kile kile kama msimu uliopita, isipokuwa wameongeza nguvu zaidi baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa”
Hii inamaanisha kuwa Conte, licha ya kuendelea kuwashawishi Sunning kumzingatia katika kampeni zijazo kupitia kile ambacho ana kifanya, bado ana uwanja mdogo wa kushawishi maamuzi.
Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.



dorophina
Conte inabidi ajitahidi ili haendelee kusalia inter milan kama bado anataka kuwepo klabuni hapo
Sarah
Asante kwa taarifa
Venerose
Asanteni kwa makala
Hopemwaikuka
Kaz anayo
warda
Jamani Conte