Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne 13/04/2021 zinasema:-
Tetesi zinasema, Juventus wanampango wa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele, 23, mkataba wake utakapoisha 2022.
Tetesi zinasema,Klabu za Paris St-Germain, Real Madrid na Inter Milan zinamfuatilia winga Jesse Lingard kabla ya dirisha la Usajili halijafunguliwa mwishoni mwa msimu. Lingard, 28, anang’ara kwa sasa ambapo anachezea klabu ya West Hamkwa mkopo akitokea Manchester United.
Tetesi zinasema, Arsenal wangali na nia ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Celtic Odsonne Edouard,23, lakini wanakabiliana na ushindani kutoka Leicester. Tetesi zinasema, Manchester United wanasita kuingia katika mazungumzo na klabu ya Borussia Dortmund ya usajili wa mshambuliaji raia wa Norway Erling Braut Haaland, 20, baada ya kushindwa kuafikiana bei nafuu kwa mchezaji mwengine wa timu hiyo, Jadon Sancho mwishoni mwa msimu uliopita.

Tetesi zinasema,Licha ya kushindikana kwa mazungumzo hayo, Manchester United hata hivyo hawajafunga milango juu ya uwezekano wa kumuwinda tena Sancho mwishoni mwa msimu huu.
Tetesi zinasema, Manchester United wamehuisha nia yao ya kumsajilili kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 26. Kiungo huyo pia anafuatiliwa na Real Madrid na PSG.
Tetesi zinasema, Tottenham wanajiandaa kumsajili beki wa Bayern Munich Jerome Boateng, 32. Beki huyo wa kati ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu.

Tetesi zinasema, Tottenham wataelekeza nguvu katika kuimarisha safu yao ya ulinzi mwishoni mwa msimu, lakini itawapasa kwanza wawauze baadhi ya wachezaji wao ili kupata pesa za kusajili mabeki bora.
Tetesi zinasema, AC Milan wana nia ya kumsajili moja kwa moja beki wa kati Fikayo Tomori, 23, ambaye anaichezea klabu hiyo kwa mkopo akitokea Chelsea.
Tetesi zinasema, Juventus wanampango wa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele, 23, mkataba wake utakapoisha 2022.
Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.



dorophina
Nice update
Sarah
Ziko poa
Venerose
Safi sana
Hopemwaikuka
Zko vzur
warda
nice