Hamilton Hana Mpango Kabisa!

Nyota wa mbio za magari, Lewis Hamilton anasema halijamjia kichwani mwake wazo la kuachana na mchezo huo wa Formula One kwa siku yoyote ile. Anachangalia kwake kwa sasa ni ufanisi zaidi na kutengeneza mataji mengi ambayo ndiyo heshima kubwa kwake. Hilo ndilo jambo ambalo analifikiri kwa wakati uliopo.

Amesisitiza zaidi kwamba katika umri wake wa miaka 34 bado ana makubwa mengi ya kufanya na haoni kama kuna kitu kinamzuia yeye kufanya hivyo. Hivyo asitokee mtu akasema kwamba yeye anafikiria kutemana na kazi hiyo, sio kweli kabisa kwake kwa sababu bado anajiona ana deni la kulikamilisha kwa umri wake.

Historia anayoijenga nyota huyo hadi sasa ni ya aina yake ndani ya Formula One kwa sababu kwa takwimu alizo nazo hadi sasa anaelekea kulingana na ikiwezekana kumpiku mtu mwenye historia yake ndani ya Manuel Fangioambaye alitwaa mataji matano ya dunia ndani ya Formula One. Huku akiendelea kufukuzia rekodi ya Michael Schumacher mwenye mataji saba.

Mbali na hilo, mkataba wake na Silver Arrows unaelekea ukingoni na ikitegemewa kwamba mwaka wa 2020 atakuwa tayari amemalizana nao, lakini anatamani sana aendelee kupata nafasi ya kuwa chini na wadhamini wake hao kwa kipindi kingine kirefu zaidi ambacho yeye anatazamia kuendelea kujihusisha na mbio za magari.

Kwa hakika anajionea kwamba hakuna sababu ya yeye kuachana na mbio za magari kwa sababu bado kuna mengi ya kufanya ikiwemo; kushindana na kuchukua mataji. Lakini pia nje ya maisha halisi kuna vitu vya yeye kuvifanya nje ya usukani ambao ndio anatumia muda mwingi katika maisha yake.

Kutokana na uzoefu wake ndani ya magari ameweza kujua mengi sana ikiwemo uwezo wa magari ambayo mara nyingi anakuwa nayo kwenye mashindano kwa kuona kwamba kuna vitu makampuni hayo yanahitaji kuviongeza ili kutanua ushindani zaidi. Ameweza kuwazungumzia Ferrari, Redbull na kuona kwamba wana kitu cha kurekebisha ili kujizatiti zaidi na kuchochea ushindani mkubwa zaidi.

Acha ujumbe