Tupo katika zama ambazo, Lionel Messi hayupo katika orodha ya wafungaji bora Ulaya. Ni zama hizi ambazo Cristiano Ronaldo ameshindwa kuchukua kiatu cha mfungaji bora wa Serie A kwa misimu miwili mfululizo. Ni zama hizi ambazo Kylian Mbappe na Erling Halland hawashikiki sokoni. Ni zama hizi ambazo dunia inawaweka Alphonso Davies na Trent Alexander-Arnold juu ya Marcelo. Zama zimeenda wapi?

Ninapowaza hivi, ndio ninaamini zama zimebadilika. Muda umebadilika na dunia siyo ile tena. Siyo ile tena ya Lionel Messi kufananishwa na miungu na Ronaldo kuaminika alitengenezwa maabara. Dunia siyo ile tena. Dunia ya sasa ni hii ya Sadio Mane, Mohamed Salah na Kelvin De Bruyne. Ndiyo dunia yao hii. Walisubiri kaka zao wapite. Sasa ni zamu yao kutamba.

Ila yupo wapi Eden Hazard? Yule aliyewapa Chelsea Europa pale Baku. Yule aliyewanyima Tottenham ubingwa. Yule Hazard aliyewakokota Arsenal umbali wa mita 50 kisha akawatungua. Ameenda wapi? Yule mchezaji bora wa epl mwaka 2015. Nani anajua alipo?

Mara ya mwisho alionekana akisajiliwa Real Madrid kwa pauni 100 milioni. Kila mtu aliridhika na lile dau. Hakuna aliyekuwa na mashaka. Hata uso wa Perez haukuwa na wasiwasi, ile siku anamtambulisha mbele ya mashabiki wa Real Madrid pale Santiago Bernabeu. Alishindwa tu kuwaambia kuwa nimemleta mrithi wa Ronaldo. Ila moyoni mwake alijua hivyo. Hata mashabiki jukwaani walijua hivyo. Wakamkabidhi jezi namba 7.

Nyuma aliwaacha mashabiki wa Chelsea na majonzi makubwa moyoni. Ila waliridhika kwa yale aliyowafanyia. Wakiamini anaenda kupata mafanikio ambayo asingeyapata kwao. Zaidi ya yote, Hazard alikuwa anaenda kuichezea timu ya ndoto zake. Isitoshe, alikuwa anaenda kufanya kazi na shujaa wake. Zinedine Zidane. Mtu aliyemfanya aupende mchezo wa soka.

Ila msimu sasa umeondoka. Hazard hajawa yule Ronaldo Real Madrid waliomdhania. Amefunga bao moja na kutoa assit 4 msimu mzima. Huyu siyo Hazard aliyemnyima Mourinho usingizi. Siyo Hazard aliyeitwa mchezaji bora baada ya Messi na Pep Guardiola. Huko ulipo Eden, tafadhali rudi maana dunia bado imelala inakusubiri uiamshe.
Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.


Adelta
Good news
@meridianbettz
Mwajumah
Asante kwa taarifa
Sauda
Hazard amebadilika sana, Ni wa leo siyo wa jana.
Antony Luseno
Kwa kipindi majina aya mawili ya messi na ronaldo yamevuma kwa kipindi kirefu katika medani ya soka
JULIANA
Yeah! nikweli Hazard wa jana si waleo,
But ikumbukwe sio kila siku ijumaa.
Zeiyana
Zama zao zimeshakwisha Ronaldo na messi wachezaji chipukizi wamekua na molali sana sikuizi
Tatu
Kila kitu kina mwisho wake zama zao zimeisha sasa zamu ya wengine mess na Ronald wakae pembeni
Dorophina
Habari njema
Janeflora malisa
Nice
Ester jackson
Kweli kabisa tarehe ,mwezi na mwaka hata siku zinabadilika hakuna sasa wale ambao walikuwa wanajulikana kwa kupokezana vijiti sasa wamekaa pembeni wamewapisha wadogo zao au wamejisahau na kuridhika walicho kipata tunashindwa kuelewa mashabiki.
rama
Maoni:kwel zama zinabadilika kabisa
Angelina
Goodupdate#meridianbet
Mwanahamisi
Habari njema
magdalena
ronaldo na messi watulie sasa ni zamu ya wenzao
Lydia Emmanuel Magoti
Hazardi jembe
Rehema
Habari njema
Warda
Kila jambo na wakati wake#Meridianbettz
Nasra
Gud news
felister
kweli zama zimebadilika
Sadick
Kupata mafanikio ktk timu moja ni jambo jingine ktk timu nyingine kwenye mfumo tofauti na Kocha tofauti. Naamini Hazard atapata mafanikio endapo atapata nafasi ya kucheza na kupona majeruhi vizuri#meridianbettz
Samiah
Habari njemaaa
Rose kapinga
Siku hazigandi Maendeleo ndio yanayotakiwa!!!
Saupha mohamed
Good news
Khadija
habari njema#meridianbettz
farida ahmadi
Hazard ni mchezaji mzuri Sana
Salma ngende
Habari nzuri
Gabriel
Hazard yuko vzur sana tatizo mfumo wa uchezaji wa Madrid auwez n wakichoyo na wakujuana na ndo maaana hata CR 7 ulimshinda kabisa
Furahav
Hazard anaitaji muda,ila naamini msimu ujao ataweza kufanya vyema.
Leonard
Hazard upepo umemkataa hispania
Issa
Hazard ni msimu mbaya kwake sana ila apambane muda anao
Hope mwaikuka
Matatzo tu akupenda
Devotha
Kila Jambo na wakati wake
Sabrina
Huu sio msimu mzuri kwa Hazard
Njiku
Zama zimebadirika cr7 na messi wanazeeka
Latifa juma mohamed
Hazard anahitaji muda,ila naamini msimu ujao ataweza kufanya vizuri zaidi.
Johnmary joel
Kweli kila majira yana matukio yake hazard sasa ni zamu yake#meridianbett
David Pere
Kwa kipindi majina aya mawili ya messi na ronaldo yamevuma kwa kipindi kirefu katika medani ya soka inabidi akaze achukue nafasi zaoo
Omary lukumbi
Zama zinaenda na nguvu pia zinapungua sasa n muda wa vijana
aisha
Ni jambo zuri sana kuona kwamba kuna wachezaji wengine ambao walikua na kiu ya kuwa kama messi na Ronaldo ni jambo la kifurahisha sana hata wao wenyewe watakua wanajidai mnoo
Caroline
Dah kweli maisha yanabadilika
Shafii
Kila nyakati zina mda wake kwa sasa messi na ronaldo ndio mwisho wao.
Neema
Habari njema
Povel
Gud update