Nyota wa Chelsea Jorginho amekiri kwamba ana ndoto ya kupata nafasi ya kufundishwa na meneja wa Manchester City, Pep Guardiola wakati fulani katika maisha yake ya soka.

 

Jorginho, Jorginho na Ndoto za Kucheza Chini ya Guardiola., Meridianbet

Jorginho amekuwa na msimu mzuri mwaka wa 2020/21 akifanikiwa kutwaa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City ya Guardiola na kushinda taji la Ubingwa wa Euro kwa Italia.

“Sikupaswa kuja Chelsea,” Jorginho alielezea katika mahojiano ya YouTube.

 

“Nilitakiwa kujiunga katika klabu nyingine. Klabu nyingine ya Uingereza. Na ikawa kama ilivyotokea na nikajiunga na Chelsea.

 

“Nikiwa na Chelsea kila kitu kilifanyika haraka sana. Nilipoona ofa yao, tayari nilikuwa London na nikasema, ‘Twende.’

 

“Je, nimewahi kuota kucheza chini ya Guardiola? Ndio. Sijui kama itatokea. Lakini ndio, ni mtu ninayemtazama.

 

“Nilipokuwa mtoto, nilitazama Barcelona yake ikishinda kila kitu na Ronaldinho, Xavi, Iniesta.” aliongeza.

Jorginho alijiunga na Chelsea msimu wa joto wa 2018 akitokea Napoli siku hiyo hiyo ambayo Maurizio Sarri alitangazwa kuwa meneja mpya wa klabu hiyo.

Akiwa mmoja wa viungo waliokamilika zaidi katika Ligi ya Premia amecheza mechi zaidi ya 170 katika mashindano yote hadi sasa na kufunga mabao 26.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa