Jurgen Klopp Abeba Tuzo ya FIFA.

Pengine wengi hawakutegemea hili lakini ni Jurgen Klopp aliyebeba tuzo ya kocha bora wa mwaka kutoka FIFA.

Jurgen Klopp alikuwa akipambania tuzo hiyo na Hans Flick (Bayern Munich) pamoja na Marcelo Bielsa (Leeds United).

Baada ya kuiongoza Liverpool kutwaa taji la EPL msimu uliopita na kuondoa ukame wa kubeba kombe hilo kwa miaka 30, Klopp amebeba tuzo ya kocha bora wa FIFA kwa mara ya pili mfululizo.

Mwaka jana Klopp alibeba tuzo hiyo baada ya kuiongoza Liverpool kutwaa kombe la Ligi ya Mabingwa – UEFA.

Ukilinganisha mafanikio ya Klopp na wapinzani wake katika kipengele hicho, huwezi kumdhania Mjerumani huyu kama angebeba tuzo hiyo.

Hans Flick alitwaa mataji yote ya Ligi ya soka Ujerumani pamoja na UEFA alipoiongoza Bayern Munich na kumaliza msimu uliopita kwa kubeba makombe matano.

Marcelo Bielsa alifanyakazi kubwa kunako mashindano ya Championship nchini Uingereza na kuifaipandisha Leeds United kwenye ligi kuu – EPL baada ya kuibuka vinara wa Championship.

Klopp alipotangazwa kocha bora wa mwaka.

Usilolijua ni kwamba, wakati mchakato wa kutafuta wagombea wa tuzo hizi unaanza (Julai 20,2019) , Hans Flick hakuwa kocha mkuu wa Bayern Munich bali alikuwa ni msaidizi wa Niko Kovac na hivyo hakuwa ametimiza muda unaotakiwa kuzingatiwa ili kupata tuzo ya kocha bora.

Hata Jurgen Klopp mwenyewe alitegemea Flick angepatiwa heshima hiyo lakini haikuwa hivyo.

Akizungumza wakati wa utoaji wa tuzo hizo, Klopp alisema ” Nimeshtuka. Nilikuwa nimekaa hapa kwa sababu mwaka jana nilishinda kwa hiyo ninawapa heshima watu wote kwa kuwa nilichaguliwa kuwania (tuzo) na nimejitokeza kwa lolote.”

Baada ya kuambiwa kuwa yeye ndiye Kocha Bora wa FIFA wa Wanaume, Klopp alisema “Hapana, lakini nimeshinda tuzo, hiyo inatosha.”

Klopp anashikilia usukani wa msimamo wa EPL kwa alama 3 zaidi ya Tottenham ya Jose Mourinho.


BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!

INGIA MCHEZONI!

16 Komentara

    Congrats to u Jurgen klopp

    Jibu

    Jurgen klopp ni kocha mwenye mfano mzuri wa kuigwa

    Jibu

    🔥🔥🔥

    Jibu

    Nic

    Jibu

    Ongera yake jurgen

    Jibu

    Hongera mwamba klopp

    Jibu

    Klop kocha

    Jibu

    klopp 👏

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safiii sana

    Jibu

    vzr

    Jibu

    Hongera

    Jibu

    Hongera sana klopp

    Jibu

    klopp sasa hivi anajisikia sana

    Jibu

    Hongera yake

    Jibu

    Pongezi kwake

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.