Kuna kitu kimoja Harry Kane kwa sasa anahitaji. Anahitaji kuamua anataka akumbukwe kama nani. Gwiji Edo Kumwembe alisema, anatakiwa kuchagua kuwa shetani au malaika.
Miezi mitatu ijayo atakuwa na miaka 28. Kama anahitaji kuondoka Spurs, huu ndio muda sahihi, hana muda mwingine. Abaki Spurs awe gwiji wa milele, au aondoke Spurs akavae medali. Hili la pili linaonekana kuwa ‘la maana’ zaidi.

Kwa inavoonekana, Spurs haina dalili ya kuwa timu tishio kwa miaka ya usoni. Kama anataka medali, lazima akubali kuwa msaliti, aondoke katika timu iliyomlea.
Kwenye mkataba wake, amebakiza miaka mitatu na Spurs. Kwa maana hiyo timu itakayomsajili itahitaji kuvunja benki kuilipa Spurs.
Kama utamwaga pesa nyingi kwa ajili ya Kane, labda ukalipa pauni 150 milioni, basi utahitaji misimu minne bora kutoka kwake. Je Kane atakuwa katika ubora huu misimu minne ijayo??
Lakini pia timu atakayoenda, inapaswa kuwa timu ambayo imeshajengwa, Kane aende kukamilishaa tu. Timu ambayo ina uhakika wa kupigania kombe. Hayupo katika umri ambao anatakiwa asubiri timu itengenezwe. Ni timu ngapi zilizokwisha tengenezwa zinamuhitaji Kane??

Spurs wanaweza kumshawishi abaki kwasababu ana mkataba wa muda mrefu, Lakini yeye mwenyewe yupo tayari kubaki?? Ana kiu ya medali na Spurs haionekani kumpatia ‘Medali Kubwa’ siku za usoni.
Mwisho wa siku, suala la Kane naliona ni gumu sana. Kuondoka Spurs ni ngumu na kubaki Spurs ni ngumu. Tusubiri muda utoe hukumu.
Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.



Adelta
Maamuzi ni yake mwenyewe
Venerose
Kazi kwake
warda
Hahaaaa kuna mtu anaweza kuchagua kuwa shetani jamani haaaaaaa?