Kane Kuwa Mpole, Levy Hanampango Huo!

Wahenga walisema “mwenye kisu kikali, ndiye mla nyama”. Ni Harry Kane au Daniel Levy mwenye maamuzi ya mwisho kule Tottenham Hot Spurs?

Baada ya Kane kuweka wazi adhma yake ya kutaka kuondoka Spurs kwenye usajili huu kwa kile alichodai ni kutaka mafanikio ya timu (kubeba mataji), Levy amejibu mashambulizi.

Mchezaji huyo aliamua kutumia vyombo vya habari kuliongelea hilo kabla ya kuwasilisha ombi rasmi kwa uongozi wa Spurs kumuachia. Vilabu mbalimbali vinahusishwa na usajili wa Harry ikiwemo Man City, Man United na Chelsea.

Kumbe mmiliki wa Spurs, Daniel Levy anawaangalia tu wanaokukuruka na suala la usajili wa Kane ambaye kimsingi, anamkataba wa miaka 3 na Spurs. Muda uliosalia kwenye mkataba wake, hauwafanyi Spurs kupata msukumo wa kutaka kumuuza kwa haraka.

Kane

Baada ya kutangaza ujio wa Fabio Paratici kama Mkurugenzi mpya wa Michezo ndani ya Spurs, Levy amesema ” Ninachoweza kukisema kuhusu kuchoshwa kwake na kutopata mataji, ni kitu ambacho kinatuchosha wote – Mimi, wachezaji wenzake na mashabiki kwa ujumla. Wote tunataka kushinda mataji.

“Kazi moja wapo atakayoifanya Fabio atakapofika, ni kuangalia wachezaji gani tutawabakiza na wachezaji gani tutawataka watafute vilabu vingine. Kuna soko huko. Kitu gani tunakitaka na kitu gani vilabu vingine vinataka, muda mwingine sio rahisi kufikiwa. Tutafanya kilicho sahihi kwa klabu yetu.”

Kwa tamko la Levy likuhusishwa na taarifa zilizokuwa zimesambaa mitandaoni kwa siku kadhaa zilizopita kuwa, Spurs hawatopokea dau lolote chini ya pauni milioni 150 (hawataki mchezaji yeyote kuhusishwa kwenye sehemu ya malipo, ni pesa pekee) ili kumsajili Kane, huenda huo ndio msimamo wa klabu na hautobadilika kamwe.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 Komentara

    Kazi ipo

    Jibu

    Mambo moto

    Jibu

Acha ujumbe