Ole, Sasa Anthony Martial Itakuaje?

Huu ndio ule wakati ambao vilabu na wachezaji mbalimbali wanahaha sokoni. Kwa Ole Gunnar Solksjaer, anakazi ya ziada kwenye dirisha hili la uongozi. Nani anatoka, nani anaingia?

Jadon Sancho bado anahusishwa na Man United na huenda akatua Old Trafford kwenye dirisha hili la usajili. Mpaka sasa, United wapo mazungumzoni na Dortmund katika mchakato wa usajili wa Sancho, watafanikiwa au watashindwa kwa mara ya pili? Tusubiri tuone.

Kwenye safu ya ushambuliaji, licha ya Ole kumuongezea mkataba kwa mwaka mmoja Edinson Cavani. Imeripotiwa kuwa Solskjaer anamipango ya kutafuta mrithi wake wa kudumu kwenye safu ya ushambuliaji. Endapo United watasajili mbadala wa El Matador na Sancho akatua United, ni dhahiri kunawachezaji wengi hawatokua na namba kwenye kikosi cha kwanza.

Baada ya msimu mbaya, Martial ataweza kuchukua namba ya yeyote kati ya Greenwood (kushoto), Cavani (katikati) na Rashford (kulia) msimu ujao?

Anthony Martial amekuwa na msimu mbaya (2020/21) lakini pia amekuwa akisemwa sana kwa kiwango chake cha kupanda na kushuka. Kwa sasa, ukimuweka Martial apambane na Rashford, Cavani au Greenwood ni ukweli kuwa hafikii uwezo wa wachezaji hao. Ole anakazi ya kufanya maamuzi magumu katika hili.

Uwepo wa Cavani, Rashford, Greenwood, Sancho na namba 9 mwingine ni uhalisia kuwa Martial atahitaji kuondoka United kama bado anampango wa kuendelea kucheza mpira katika kiwango kikubwa na kupata namba kwenye kikosi cha kwanza.

Kuna tofauti ya pauni milioni 11 tu kati ya Man United na Dortmund katika mchakato wa usajili wa Sancho.

Inaripotiwa kuwa, wakala wa Martial ameanza kumtafutia mteja wake timu nyingine. Real Madrid ikihusishwa na mpango wa kumsajili kwa mkopo wa msimu mmoja ikiwa ni sambamba na uwezekano wa kumsajili moja kwa moja. Mpango wa wakala wa Martial unaendana na mawazo ya Ole Gunnar Solskjaer ambaye inasemekana yupo tayari kumuweka Martial sokoni baada ya kumvumilia kwa muda mrefu bila ya mabadiliko chanya.

Sasa Martial itakuaje, unasepa United au utapambania nafasi yako kwenye kikosi cha The Red Devils msimu ujao? 


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 Komentara

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Makala bomba

    Jibu

Acha ujumbe