Kiungo wa klabu ya Chelsea Ngolo Kante anatarajiwa kurudi katika klabu ya Chelsea mwezi Febuari amezungumza hivo kocha mkuu wa klabu hiyo Graham Potter.
Kiungo huyo alipata majeraha kabla ya michuano ya kombe la dunia na kukosa michuano hiyo, Lakini ilitarajiwa kua kiungo huyo atarejea mapema ndani ya klabu hiyo ila ameonekana bado hajawa fiti kuanza kucheza ndani ya klabu hiyo.
Kiungo Ngolo Kante ambaye amekua mchezaji muhimu ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kucheza kwa kiwango cha juu ndani ya klabu hiyo pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa, Lakini kwa siku za karibuni amekua akipatwa na majeraha ya mara kwa mara.
Kocha wa klabu ya Chelsea Graham Potter amethibitisha kiungo huyo atarejea ndani ya klabu hiyo mwezi Febuari, Kurejea kwa kiungo huyo ndani ya timu hiyo kutaimarisha klabu ya Chelsea ambayo imekua ikitetereka siku za hivi karibuni.
Klabu ya Chelsea imekua ikipata changamoto tangu kuanza kwa msimu huu na kudondsha alama mara kwa mara, Na hii inatokana na kupata idadi kubwa ya majeraha kwenye kikosi chao hivo klabu hiyo inajitahidi wachezaji wake wawe fiti na miongoni mwao ni Kiungo Ngolo Kante ambaye amekua mhimili mkubwa kwa timu hiyo.

