N’golo Kante: Inaripotiwa kuwa anaweza kuondoka Chelsea msimu ujao kama mchezaji huru baada ya kukataa kandarasi mpya Stamford Bridge. Kante ambaye ni kiungo wa timu ya Taifa ya Ufaransa ana miaka 31 mpaka sasa. Lakini mazungumzo yanaendelea.

 

Kante Akubali Kuongeza Mkataba

Mazungumzo yamekuwa yakiendelea kati ya mchezaji na klabu kwa zaidi ya miezi 12 lakini kutokana na Kante kuwa nje ya uwanja mara nyingi kumefanya mazungumzo kuwa magumu zaidi. Kulingana na Athletic kiungo huo amesikitishwa na na pendekezo la The Blues la kumpa mkataba wa miaka miwili na chaguo la tatu ikiwa klabu itaamua kuongeza muda.

Baada ya kumuona mlinzi mpya na mchezaji mwenzake Kalidou Koulibaly mwenye umri wa miaka 31 akipewa mkataba wa miaka minne. Kante anaamini kwamba ofa kama hiyo inatakiwa kutolewa kwake.

 

Kante Akubali Kuongeza Mkataba

Licha ya kiungo huyo kuwa mtu maarufu sana katika klabu hiyo, Chelsea wana mashaka juu ya rekodi ya jeraha la mchezaji huyo wa zamani wa Leicester City. Tatizo la paja limemfanya akosekane tangu katikati ya  Agosti muhula huu, huku akihitaji dakika zake kusimamiwa kwa uangalifu msimu 2021/2022 kutokana na matatizo ya goti na nyama za paja.

Kante amecheza mechi 262 akiwa na The Blues, akishinda taji la ligi kuu ya Uingereza, Ligi ya Mabingwa, Ligi ya Europa, Kombe la Dunia, Kombe la FA, Kombe la Super Cup la Ulaya. Pia alikuwa ni sehemu muhimu ya kikosi muhimu cha Les Bleus kilichoshinda Kombe la Dunia chini ya Didier Deschamps mnamo mwaka 2018.

 

Kante Akubali Kuongeza Mkataba

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa