Nadal Asema alitokwa na Machozi Messi alipofunga bao la tatu

Mchezaji nguli wa tenesi duniani raia wa kimataifa wa Hispania Rafae Nadal amesema alitokwa na machozi pale mchezaji Lionel Messi alipofunga bao la tatu katika mchezo wa fainali dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa.

Licha ya ushabiki wake mkubwa wa klabu ya Real Madrid lakini alitokwa na machozi ya furaha baada ya staa huyo wa Argentina kufunga bao la tatu kwenye mchezo huo, Kwani alijua kabisa kua anaenda kupata kila kitu ambacho alikipigania kwa muda mrefunadalMchezaji Nadal ambaye ameshinda mataji 22 makubwa ya Tenesi duniani anasema kua alipoona Messi amefunga bao hilo aliona kabisa mcheezaji huyo anakwenda kupata kile ambacho amekua akikipigania kwa muda mrefu na akakikosa.

Gwiji huyo pia alizungumzia ubora wa kijana Kylian Mbappe kwenye mchezo wa fainali baada ya kuonesha ubora mkubwa katika mchezo wa fainali, Na kusema kua mchezaji huyo alionesha ubora mkubwa sana.nadalGwiji Rafael Nadal pia alizungumzia suala la Mbappe kuikataa Real Madrid na kusaini mkataba mpya na PSG ambapo gwiji huyo amefunguka kua mchezaji huyo kama atakuja ndani ya Real Madrid sio mbaya kwani vitu vinatokea na kubadilika muda mwingine.

Acha ujumbe