Nyota KMC aanza kutupia ligi kuu

Nyota wa zamani wa Azam ambaye kwa sasa anakitumikia kikosi cha KMC, Awesu Ally jana alhamis amefanikiwa kufunga bao lake la kwanza kwenye ligi msimu huu dhidi ya Polisi Tanzania.

Mchezo huo ulipigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar, ulimalizika kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yakifungwa na George Makang’a na Awesu Ally.

Nyota KMC aanza kutupia ligi kuu

Baada ya ushindi huo KMC wamefanikiwa kufikisha pointi 22 baada ya kucheza mechi 17, wakishika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi.

Nyota KMC aanza kutupia ligi kuu

Kikosi hicho kinatarajia kucheza mchezo mwingine wa ligi dhidi ya Simba, Desemba 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Acha ujumbe