Karim Benzema jana amefanikiwa kutangazwa kama mshindi mpya wa tuzo ya Ballon Dor inayotolewa na jarida la Ufaransa maarufu kama France Football. Tuzo hii hutolewa kwa mchezaji aliefanya vizuri zaidi kwa msimu huku imtambua mchezaji fulani kua bora zaidi duniani kwa msimu husika.
Kijana kutoka mitaa ya Lyon pale Ufaransa imemchukua miaka miaka 34 kufikia ndoto yake aliyokua akiiota kila siku mchezaji huyo aliesajiliwa klabu ya Real Madrid mwaka 2009 akija na wachezaji kama Cristiano Ronaldo, Ricardo Kaka, pamoja na Xabi Alonso huku mchezaji huyo hakupewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwani wenzake Kaka na Ronaldo tayari walishabeba Ballon Dor.
Benzema yeye hakuwahi kua na kinyonge wala wivu pale wenzake walipofanya vizuri zaidi yake miaka tisa ya Ronaldo ndani ya Real Madrid Karim Benzema alikua akiishi chini ya kivuli cha staa huyo ndio maana haishangazi kuona Benzema amehusika kwenye pasi nyingi za mabao kwa Ronaldo kuliko mchezaji yeyote ndani ya Real Madrid.
Kijana huyo kutoka mitaa ya Lyon mwenye asili ya Algeria alikua na msimu bora sana katika mwaka 2021/22 baada ya kuisaidia timu yake kubeba mataji matatu ligi ya mabingwa ulaya,La liga, Spanish Super Cup huku akimaliza kama mfungaji bora wa ligi ya mabingwa barani ulaya, pamoja na ligi kuu ya Hispania.
Jana rasmi mchezaji huyo kapewa tuzo ya Ballon Dor akiwa na umri wa miaka 34 mchezaji mkubwa kubeba tuzo baada ya miaka 66 hii inakua baada ya miaka 14 ndani ya klabu ya Real Madrid huku tayari wachezaji wenzake wawili wakiwa tayari walishashinda tuzo hiyo mara tano klabuni hapo Ronaldo mara nne huku Luca Modric akibeba mara moja.
Kupitia Karim Benzema inatoa funzo kwa kila mmoja kua tujifunze kuwapongeza na kuwapigia makofi wenzetu pale wanapofanikiwa kwani siku zetu zinakuja mbeleni na wakati wa mungu ni wakati sahihi kwani Benzema aliishi kuwapobgeza wenzake mpaka pale wakati wake ulipofika.

