Klopp Aamini Nunez Yupo Fiti Asilimia Mia Kwasasa.

Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp anaamini mshambuliaji wake raia wa Uruguay Darwin Nunez yupo fiti kwa asilimia mia kwasasa.

Klopp ameyazungumza jana baada ya mshambuliaji huyo kufunga bao pekee lililoipa klabu hiyo alama tatu muhimu klabu hiyo dhidi ya klabu ya West Ham katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza huku likiwa goli lake la kwanza katika uwanja wao wa nyumbani Anfield.kloppStaa huyo aliesajliwa kutoka klabu ya Benfica ya nchini Ureno kwa rekodi ya usajili huku tangu ajiunge klabuni hapo amekua hana mwendelezo wa kiwango lakini kwasasa anaonekana kuanza kuonesha ubora wake aliokua nao ndani ya klabu ya Benfica.

Darwin Nunez tayari amefunga magoli matano kwenye michezo 12 aliyocheza klabuni hapo huku akiwa amefunga magoli matatu kwenye michezo minne iliyopita ya michuano yote klabuni hapo.kloppKlopp ameleeleza mshambuliaji wake huyo sasa ni kama yuko sawa kwa asilimia baada ya kuanza kwa kusuasua “Amefika kwa asilimia mia, hata ukiangalia namba zake ni nzuri”

 

Acha ujumbe