Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp anaamini kuwa kocha mwanzake ambaye anainoa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ni moja ya kocha bora duniani kwa sasa
Makocha hao waiwili wanatarajia kukutana kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza siku ya jumapili, ambapo Pep Guardiola atamkarubisha Jurgen Klopp kwenye dimba la Etihad, huku kikosi cha Liverpool kikiwa nyuma kwa alama moja dhidi ya Man city ambaye anaongoza ligi hiyo.
Jurgen Klopp akiongea kwenye mtandao wa klabu ya Liverpool alisema, “naheshimu sana ambacho klabu ya Man city wanafanya, ni timu ya ajabu kwenye mpira wa miguu, na kwangu mimi, Pep ni kocha bora wa dunia.
“Muunganiko wao unakufanya uchanganyikiwe, lakini, habari njema ni kuwa na wao ni binadamu pia, kama ningekuwa mtu wa tofauti, huenda ningekuwa nina msongo kidogo kuhusu jinsi Pep Guardiola anavozifundisha hizi timu.
“Huenda wakati nipo Borussia Dortmund tungeshinda makombe mengi zaidi kama Pep asingekuwepo Bayern Munich, ni sawa na sasa fikilia kuwa kama asingekuwepo hapa huenda tungeshinda makombe mengi zaidi ya ligi, lakini sio kama hivi, asante mungu, nina furaha.”
Klopp na Pep pia wanatarajia kukutana tena kwenye mchezo wa nusu fainali ya FA Cup April 16 kwenye dimba la Wembley.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.