KOCHA SIMBA AANZA NA GIA HII HUKO MISRI

FADLU Davids Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kazi kubwa iliyopo kwa sasa ni kuwaandaa wachezaji kuwa tayari kwa ushindi kwenye mechi zao za ushindani zijazo.

Kuelekea msimu wa 2024/25 Simba imeweka kambi Misri ikiwa na wachezaji kama Mzamiru Yassin, Zimbwe, Ally Salim na ligi inatarajiwa kuanza Agosti 16 2024 huku mabingwa wakiwa ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Simba ni wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa ambapo ni katika Kombe la Shirikisho Afrika huku zipo timu mbili kutoka Tanzania nyingine ni Coastal Union.SIMBAFadlu amebainisha kuwa mazoezi ambayo yanafanyika ni maalumu kwa kuwa na kikosi cha ushindi kitakachowapa matokeo chanya katika mechi za msimu wa 2024/25.

“Kikubwa ni kuona kwamba tunawapa mbinu za kutafuta ushindi uwanjani hili litaongeza uwezo wao zaidi na kuwa wapambanaji kwenye mechi za ushindani ambazo tutacheza.

“Mashabiki wa Simba wanahitaji kuona matokeo yakipatikana hivyo ni muhimu kuwa pamoja nasi kwenye mechi zote na wachezaji wanatambua kwamba jambo la msingi ni kufanya vizuri.”

Acha ujumbe