Vilabu vikubwa vya England, Manchester City, Liverpool na Chelsea vinatajwa kuwania saini ya beki wa FC Barcelona, Jules Koundé, kuelekea dirisha la usajili la majira ya joto. Licha ya kuwa na mkataba hadi 2030, klabu hizo zinaonekana tayari kujaribu bahati yao.

Taarifa zinaeleza kuwa Manchester City tayari wamefanya mawasiliano ya awali kuulizia upatikanaji wake, huku Chelsea wakiwa na historia ya kumtaka tangu akiwa Sevilla FC. Liverpool nao wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya beki huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja.
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Deco, amethibitisha kuwa kuna mawasiliano kutoka kwa vilabu vikubwa, lakini hakuna ofa rasmi iliyowasilishwa hadi sasa. Ameweka wazi kuwa klabu haipo tayari kumuachia kirahisi, ingawa hali ya kifedha inaweza kuathiri maamuzi yao.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Koundé amekuwa mhimili muhimu chini ya kocha Hansi Flick, akicheza mechi 40 msimu huu. Hata hivyo, Barcelona wanahitaji fedha kwa ajili ya kusajili majina mapya kama Julián Álvarez na Alessandro Bastoni, jambo linaloweza kuwafanya wafikirie kumuuza iwapo dau kubwa litawasilishwa.

Inatajwa kuwa thamani yake inaweza kufikia euro milioni 80, kiwango ambacho kinaweza kuwavutia wanunuzi. Katika kipindi hiki muhimu cha msimu, Koundé atakuwa chini ya macho ya wengi, hasa katika mechi za La Liga na Ligi ya Mabingwa, ambazo zinaweza kuamua hatma yake msimu ujao.

