Kylie Walker 50/50 Kukipiga Dhidi ya Arsenal

Beki wa kulia wa klabu ya Manchester City na nahodha wa klabu hiyo Kylie Walker bado haijajulikana kama ataweza kuwepo katika mchezo dhidi ya klabu ya Arsenal siku ya Jumapili.

Kylie Walker alipata majeraha akiitumikia timu ya taifa ya Uingereza katika mchezo dhidi ya mabingwa mara tano wa dunia timu ya taifa ya Brazil, Majeraha ambayo yamemuweka mguu ndani mguu nje kuelekea mchezo dhidi ya Arsenal siku ya jumapili.kylie walkerBeki huyo amekua moja ya wachezaji muhimu zaidi kwenye kikosi cha Manchester City kwa misimu takribani sita sasa, Hivo kukosekana kwao katika mchezo huo dhidi ya Arsenal siku ya Jumapili itakua pengo kubwa kwa Man City.

Mchezo dhidi ya Arsenal utakua moja ya michezo migumu sana msimu huu kwa City kwani mchezo huo utatoa taswira ya mbio za ubingwa msimu huu, Kwani mpaka sasa klabu ya Man City wanakamata nafasi ya tatu hivo mchezo huo unaweza kuwapa nafasi ya kurejea kileleni.kylie walkerKama Kylie Walker atakosekana katika mchezo huo ni wazi kocha Pep Guardiola atalazimika kucheza na mabeki watatu au kumchezesha moja ya mabeki wa kati katika eneo la pembeni na mara kadhaa amekua akipendelea kumtumia Manuel Akanji au Nathan Ake.

Acha ujumbe