Beki wa kulia wa klabu ya Manchester City Kylie Walker amemmwagia misifa beki wa kulia wa klabu ya Bayern Leverkusen vinara wa ligi kuu nchini Ujerumani Jeremie Frimpong.
Kylie Walker wakati akifanya mazungumzo jana alisema ” Nani anacheza beki wa kulia pale Leverkusen ambaye alikua Man City, Mungu wangu amefunga magoli mangapi? maajabu”Hayo yalikua maneno ya beki huyo wa zamani wa Tottenham akimzungumzia beki huyo wa Leverkusen ambaye amewahi kupita ndani ya Manchester City kwa kipindi cha takribani miaka tisa akiwa timu ya vijana, Huku kwasasa akiwa anafanya vyema sana ndani ya kikosi cha Bayern Leverkusen.
Jeremie Frimpong hajasifiwa kwa bahati mbaya kwani amekua na msimu bora sana ndani ya kikosi cha Bayern Leverkusen chini kocha Xabi Alonso, Kwani amekua moja ya wachezaji waliohusika kwenye mabao mengi ndani ya kikosi hicho.Beki Jeremie Frimpong amekua kwenye kiwango bora sana msimu huu kando ya beki mwenzake ambaye anacheza kushoto Alex Grimaldo, Frimpong mpaka sasa amehusika kwenye mabao 21 ambapo amefunga mabao 11 huku akipiga pasi 10 za upatikanaji wa mabao hii inadhihirisha kauli ya Kylie Walker kwamba beki huyo amekua bora sana msimu huu.