Bingwa mara saba wa michuano ya langalanga Lewis Hamilton raia wa Uingereza ametunukiwa uraia wa heshima wa taifa la Brazil, Dereva huyo alitunukiwa uraia huo jana jumatatu kwenye baraza la manaibu jijini Brasilia.

Hii imekuja kutokana na wabrazil kufurahishwa na dereva huyo ambae alishikilia bendera ya nchi hiyo alipopata ubingwa wake huko Interlagos mwaka jana kitu kilichowafurahisha zaidi raia wa nchi hiyo pamoja na uongozi wa nchi hiyo pia.lewis hamiltonLewis Hamilton bado anatafuta ushindi wake wa kwanza kwenye michuano ya mwaka huu ambayo bado haijamuendea vizuri sasa, Lakini alionekana kua na tabasamu pana sana jana wakati akitunukiwa uraia huo wa heshima.

“Ningependa kusema asante kwa kila mtu hapa kwa wale wote waliopambana kwa kila njia kufanikisha hili, Kwa kweli ni heshima kubwa kwangu nikiwa hapa kuupokea na kuukubali uraia huu na sasa najihisi mimi ni mmoja wenu” Alisema Lewis Hamiltonlewis hamiltonDereva huyo pia aliendelea kuonesha furaha yake na kueleza kua amekua na mapenzi makubwa kwa taifa la Brazil tangu alipofika nchini hapo kwa mara ya kwanza mwaka 2007.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa