Klabu ya Liverpool imethibitisha kumsajiri mshambuliaji wa klabu ya Benfica Darwin Nunez kwa kuvunja rekodi ya  klabu hiyo kwa kitita cha thamani £87million.

Mshambuliaji huyo amesajiriwa kutoka Benfica kwa uhamisho wa thamani ya £70milion, huku kukiwa na kipengere cha £17million, ikiwa atapata mafanikio na klabu ya Liverpool basi watapaswa kulipa hicho kiasi ili kukamilisha uhamisho huo.

Liverpool

 

Awali klabu ya Manchester United nayo ilikuwa inawania saini ya mshambuliaji huyo, kabla ya Liverpool kufanikisha uhamisho huo. Nunez amekabidhiwa jezi namba 27 na amesaini kandarasi ya miaka 6.

“Kiukweli nina furaha kuwa hapa kwenye klabu kubwa ya Liverpool. Ningependa kuwashukuru mtu wangu wa karibu, wazazi wangu na mwanangu, ambaye yeye ndio chanzo cha mimi kufanya zaidi.

“Imekuwa hatua muhimu kwangu kwenye maisha yangu ya soka, kiukweli najivunia wao na kazi niliyoifanya mimi na mwenza wangu, kama timu na namshukuru yeye mimi kuwa hapa. alisema Darwin Nunez”

Nunez aliongozea; “Ni sifa kubwa mimi kuwa Liverpool na nina furaha kuwa sehemu ya klabu hii bora. Nimecheza dhidi yao na nimewaona mara nyingi kwenye michuano ya ulaya, na aina yangu ya uchezaji nadhani naweza kupata nafasi ya kucheza.

“Ninachoweza kusema, nimeiangalia sana na ni klabu kubwa na natumai naweza kutoa kila kitu ili niweza kuisaidia timu.”


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa