Kocha kutoka Afrika ya Kusini aliyekuwa anainoa klabu bora ya karne Al Ahly Pitso Mosimane mpaka sasa yeye na benchi lake la Ufundi bado hawajasaini mkataba wa kuinoa klabu yoyote.

Awali kulikuwa na uvumi kuwa kocha Pitso Mosimane na benchi lake la ufundi, kuwa wamepata timu nchini Qatar na tayari walikuwa wameshasaini kandarasi ya kuinoa timu hiyo, kabla ya kampuni inayomsimia kutoa waraka wa kupinga madai hayo.

Pitso Mosimane

“14 june 2022 kumezuka tetesi ambzo zinamhusu mteja wetu Pitso Mosimane, kuwa yupo Qatar na kumsingizia kuwa tayari ameshasaini kandarasi mpya na timu mpya.

“Mt sports Marketing and management ingependa kueleza kuwa tetesi hizo ni upotoshaji na sio kweli. Kocha Pitso na benchi lake la ufundi hawajasaini na timu yoyote, na atarejea nchini afrika kusini baada ya kumaliza mambo yake.

“Tangu aachane na klabu yake ya zamani, tumepokea offer nyingi kutoka timu mbalimbali za kimataifa na timu za ndani zikiwepo za taifa. Bado hatujafanya maamuzi yoyote.

‘Maendeleo yoyote kuhusu swala hili, Mt sports Marketing and management ndio watatoa tamko rasmi.” Waraka wa Mt sports Marketing and management ulisomeka hivyo.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa