Klabu ya Liverpool yenye makao yake makuu Anfield yaongoza kwenye mbio za kumuwania mchezaji wa Borrusia Dortmund Jude Bellingham huku ikiipita Manchester United kwenye mbio hizo za kumuwania mchezaji huo.

 

Liverpool Yaongoza Kumuwania Bellingham

 

Mchezaji huyo ana orodha ndefu ya mashabiki nchini Uingereza kutokana na aina ya uchezaji wake huku akiisaidia timu yake hiyo ya Bundesliga kupata bao juzi dhidi ya UEFA dhidi ya Manchester City ambapo walipoteza kwa mabao 2-1.

Mkataba wa mchezaji huyo unaendelea hadi 2025, ambapo Bellingham alihama kutoka Uingereza alipokuwa akicheza katika timu ya Birmingham City na kwenda Ujerumani kuwatumika Dortmund mnamo 2020.

Liverpool Yaongoza Kumuwania Bellingham

 

Liverpool wanaongoza katika mbio za kumsajili kinda Bellingham kutoka Borrusia kuliingana na ripoti ya Telegraph, Wakati huo huo United nao pia wanavutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19, ambaye ameanza mechi zote 9 za msimu huu akiwa Dortmund. Bellingham anaweza kuruhusiwa kuondoka katika klabu hiyo mwaka 2023 na klabu hiyo ya Ujerumani inasubiri ofa kutoka kwa Majogoo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa