Luis Nani ni jina lenye heshima kubwa miongoni mwa majina ya wachezaji waliowahi kuitumikia Manchester United. Nani ni mchezaji aliyerithi mikoba ya Cristiano Ronaldo na aliitendea haki kwa nafasi yake.

Mwaka 2008 wakati ambapo Man United walibeba kombe la Ligi ya Mabingwa, Luis Nani alikuwa miongoni mwa wachezaji waliopeleka mafanikio hayo Old Trafford, hii inakwenda sambamba na makombe mengine mengi aliyoyapata akiwa na Man United.

Luis Nani, Luis Nani Azungumzia Uwezo wa Fernandes., Meridianbet
Ronaldo (kushoto) akishangilia Kombe la UEFA 2008 akiwa na Nani (kulia)

Nani aliwahi kucheza timu moja (Sporting Lisbon) na Bruno Fernandes kwa msimu mmoja – 2018/19 kabla hajatimikia Marekani ambapo anaichezea timu ya Orlando City mpaka sasa.

Alipokuwa Sporting, Nani aliwahi kumshauri Fernandes kujiunga na EPL tena kama atapata nafasi ya kujiunga na Manchester United basi asifanye makosa, aitumie nafasi hiyo. Fernandes alifanya kweli mwezi Januari, 2020 na kuanzia hapo imekuwa ni safari ya mafaniko kwake.

Mpaka sasa, Fernandes amehusika kwenye magoli 34 ya United – amefunga 21 na kutoa pasi 13 za magoli. Takwimu zinaonesha, hakuna mchezaji yeyote kwenye mpira wa Uingereza aliyehusika kwenye magoli mengi kumzidi Bruno (Kane 31, Son 25, de Bryune 23 na Salah 22) tangu alipojiunga na EPL mwezi Januari.

Akizungumza na United Review, Luis Nani ameshangazwa na uwezo wa Man United kwa kipindi kifupi alichokuepo kwenye timu hiyo.
Luis Nani, Luis Nani Azungumzia Uwezo wa Fernandes., Meridianbet
Bruno Fernandes (kushoto) alipokuwa anacheza Sporting Lisbon na Nani (kulia).

Luis Nani anasema ” miaka kadhaa iliyopita nilimpa ushauri Bruno Fernandes, wakati ule nilikuwa nikicheza naye Sporting Lisbon. Bruno kwa sasa ni mchezaji mzuri zaidi kuliko kipindi ambacho tulikuwa tunacheza pamoja. Alikuwa anafanya vizuri kwenye Ligi ya Ureno – lakini Ligi ya Ureno sio sawa na Premier League, kwenye kila kitu kunaugumu na ubora mkubwa.

“Niliuona uwezo mkubwa kwa Bruno na nilimshauri aende Uingereza kama atafikiria kubadilisha ligi. Nilimwambia , ‘Uchezaji wako utafaa sana kule na mashabiki watapagawa na uwezo wako’

“Aina ya uchezaji wake ni kitu ambacho mashabiki wanakikubali. Ni mchezaji ambaye anapenda kuchukua maamuzi magumu, anabeba majukumu kwenye mchezo, anatoa pasi ngumu na kupiga mashuti. Haogopi kufanya makosa, anafikiria mafanikio na kuifanya timu ifanikiwe. Anajua faida ya kufanya hivyo, hiyo ndio Man United.

Bruno amefanya makubwa sana mpaka sasa, amefunga na kutengeneza magoli mengi lakini ninadhani ataendelea kuwa bora zaidi na kuisaidia timu kupata mafanikio zaidi.”


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

16 MAONI

  1. Bruno amefanya makubwa sana mpaka sasa, amefunga na kutengeneza magoli mengi lakini ninadhani ataendelea kuwa bora zaidi na kuisaidia timu kupata mafanikio zaidi

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa