Vita ya kuiwania saini ya staa wa Dortmund Erling Haaland sio ndogo na inaendelea kwa kasi kubwa. Staa huyu anatarajiwa kuondoka Dortmund kiangazi huku Barcelona na wapinzani wao Real Madrid wakiipania saini yake.

Kwa mujibu wa Bild kupitia Marca, Barcelona wanaonekana kutokuwa nabahati kwenye kuwania saini ya staa huyu. Real Madrid pia hawapo peke yao wanaohusishwa na kuwa karibu zaidi na saini ya Haaland.

Vinara wa Ligi Kuu Uingereza, man City nao wanatajwa kuwa unyayo kwa unyayo na Real, wakiwa na matumaini makubwa ya kuinasa saini hii.

Windo limekuwa tafu sivyo?

Xavi Hernandez anaripotiwa kukutana na Haaland wiki iliyopita kule Munich, na hakuna mashaka kuwa staa huyu ni kipaumbele cha Barcelona kwenye dirisha lijalo la uhamisho.

Lakini kwa Real Madrid wao tayari kipaumbele chao kinatajwa kuwa ni Kylian Mbappe kutoka PSG, lakini Haaland pia yupo katika vitabu vyao. City pia wanatajwa kuwa windoni baada ya kukwama kumnunua Harry Kane kutoka Tottenham.

Haaland akiwa na umri wa miaka 21 tu tayari amefunga magoli 80 kwenye mechi zake 79 akiwa na Dortmund tangu alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2020.


VUNA MKWANJA NA SHINDANO LA EVOPLAY SPRING AWEKING

Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000  katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa