Kocha wa klabu ya Liverpool Jürgen Klopp amedai kuwa timu ya Manchester City wangetawazwa mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza mwezi wa pili kama klabu ya Liverpool isingekuwepo
Man City na live pool ndani ya miaka minne wamekuwa wakibadilishana mataji kati yao City akiwa amechukuwa mara tatu, Liverpool akiwa amechukua mara moja, huku wakiwa wanafukuzana kwenye mbio za ubingwa mwaka huu, ambapo Pep na timu yake wako kileleni kwa point sita, wakati Klopp na timu yake wana mchezo mmoja mkononi wakiwa nafasi ya pili.

Klopp wakati akizungumza na waandishi wa habari alinukuliwa akisema, “ni ligi ngumu duniani, hakuna shaka kwenye hilo, lakini ni changamoto, na hakika tunafurahia, kama tusingekuwepo hapa mwaka huu au miaka miwli iliyopita au mitatu basi Man City angekuwa bingwa mwezi February.
“Sababu tupo hapa, ni ngumu. Kama City wasingekuwepo hapa nadhani tungekuwa na nafasi ya kuwa mabingwa.”
Awali Guardiola aliwai kuiita timu ya Liverpool kuwa ni washindani imara ambao hajawai kukutana nayo tokea aanze kazi yake ya kuwa mkufunzi, na Klopp nae amesema sawa sawa kuhusu City na kutoa sifa zake kwa kocha huyo.
Aliongezea Klopp, “ningeweza kusema City ni timu ngumu niliyowai kukutana nayo, lakini siwezi kusahau nulishindana nae tayari akiwa Bayern na siwezi kusema kuwa ilikuwa rahisi.
“Najua nini anamaanisha tunasukumana kwenye hatua za juu kwenye miaka hii michache, na kiasi cha pointi ambacho tunakusanya, sawa, hatukuweza kwenda sawa mwaka uliopita kwa sababu fulani fulani, lakini kwa miaka mingine tulikuwepo nyuma.
‘Sidhani kama City wangeweza kupata idadi ya pointi ambazo walizipata kama tusingekuwepo, na kama wasingekuwepo ingekuwa sawa kwetu, lakini kuna michezo mngi ya kucheza tutaona wapi tutaishia.”
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


