Bruno Fernandes amedokeza kwamba Cristiano Ronaldo bado anatafuta kuondoka Manchester United kabla ya kumalizika kwa dirisha la usajili.

ronaldo, Majibu ya Bruno Fernandes Alipoulizwa Kuhusu Ronaldo Kuondoka Man Utd., Meridianbet

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 amekuwa akitafuta klabu mpya msimu huu wa joto lakini licha ya wakala wake, Jorge Mendes, kufanya mazungumzo na vilabu kadhaa barani Ulaya vikiwemo Chelsea, Bayern Munich na Atletico Madrid, lakini bado haijajulikana ni wapi haswa Ronaldo ataenda.

Ronaldo ameanza msimu mpya huko United lakini hata mechi ya jana dhidi ya Liverpool hakucheza, mabao ya Jadon Sancho na Marcus Rashford yaliipatia United ushindi wa 2-1 dhidi ya kikosi cha Jurgen Klopp, huku Ronaldo akikaa kwenye ubao kama mchezaji wa akiba.

ronaldo, Majibu ya Bruno Fernandes Alipoulizwa Kuhusu Ronaldo Kuondoka Man Utd., Meridianbet

Fernandes, ambaye pia anacheza pamoja na Ronaldo katika timu ya taifa ya Ureno, amewataka mashabiki kuheshimu uamuzi wa nyota huyo kuhusu mustakabali wake na kusisitiza kuwa “angefurahi kibinafsi” ikiwa hiyo ingemaanisha kuondoka United kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Kuna uvumi mwingi lakini hakuna aliye bora zaidi kuliko Cristiano kuzungumzia hilo, Fernandes aliiambia Eleven Sports alipoulizwa kuhusu mustakabali wa Ronaldo.

Naweza kujua jambo moja au mawili, lakini sitakuwa mtu wa kusema, Cristiano ni mtulivu, alifanya mazoezi vizuri wiki hii, alifanya kazi yake kama ambavyo amekuwa akifanya, ataendelea kufanya hivyo. Kwa sasa yeye ni mchezaji wa United, sijui kuhusu mustakabali wake, kama ataondoka au hataondoka. Kama alivyosema, atazungumza hivi karibuni na watapata wakati wa kusikia maneno yake na kile anachosema”.

“Lazima tuheshimu anachotaka kufanya, chochote anachotaka kufanya, ikiwa atabaki, tutafurahi juu yake, ikiwa ataondoka kwa sababu anaona ni bora kwake, nitakuwa na furaha kwake, Jambo muhimu zaidi ni kwamba yeye ni sawa, katika ngazi ya juu na kufanya nchi yetu kujivunia

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa