Ni miezi miwili yenye michezo ambayo pengine, itaamua msimu wa Man United utakavyokuwa kufikia Disemba, 2021. Sema kimeumana!
Katika michezo 7 ya EPL, United ameambulia pointi 14 tu. Akiwa amepoteza mchezo 1, katoa sare 2 na kushinda 4. Usajili wa wachezaji nyota – Cristiano Ronaldo, Jadon Sancho na Rafael Varane, ni kama haujazaa matunda mpaka sasa.
Ole Gunnar Solsksjaer anakila kitu anachokihitaji kama kocha wa Man United, pengine anakosa kiungo mkabaji tu. Lakini, hii haimaanishi United wanashindwa kupata matokeo kwa sababu hiyo.
Yote 9, 10 ni michezo 10 ya United inayofuata kwa mwezi Oktoba na Novemba. United ataingia uwanjani kuchuana na vigogo wote wa EPL ndani ya miezi hii. Habari mbaya zaidi, ni majeruhi kwa wachezaji wawili tegemezi kwenye safu ya ulinzi – Harry Maguire na Rafael Varane.
Uwepo wa Maguire na Varane kama walinzi wa kati, kwa kiasi fulani umeimarisha safu ya ulinzi ya United na sasa, United inawakosa wachezaji hawa kwa michezo kadhaa ijayo.

Kukosekana kwa walinzi hawa, kunawapa nafasi Victor Linderlof, Erick Bailly na Phil Jones kuingia kwenye kikosi cha kwanza. Kitu kinachowazisha ni, walinzi hawa hawana historia nzuri ya kupata matokeo wanapocheza pamoja.
Katika michezo 5 ambayo Lindelof na Bailly wamecheza pamoja, United waliambulia kupata kadi nyekundu, majeruhi, kuzidiwa mbinu, kutoruhusu goli na kupoteza mchezo. Kwa Jones, anazaidi ya siku 365 hajacheza mpira kutokana na majeruhi.
Hali ni mbaya kwa Man United wakati huu ambao watacheza dhidi ya Leicester City, Atalanta, Liverpool, Spurs, Man City, Watford, Villarreal, Chelsea na Arsenal ndani ya miezi miwili.
Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

CHEZA HAPA

