Klabu ya Manchester United imeongeza mkataba wa nyota wake Jesse Lingard kwa kupitia kipengele kwenye mkataba wake kinachowaruhusu kuongeza mkataba wa kwa mwaka mmoja.
Nyota huyu wa miaka 28, alikuwa ni sehemu ya kikosi cha Uingereza kilichofikia nusu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018, na mpaka sasa amecheza mara mbili tu pale Manchester United msimu huu akiwa chini ya meneja Ole Gunnar Solskjaer.
Mkataba wa Lingard ulipaswa kuisha msimu ujao wa joto, lakini United wameamua kuongeza mwaka mmoja na hivyo atasalia klabuni hapo hadi mwaka 2022.

Manchester United
Dili hili linaweza kutupa ujumbe kuwa klabu ina mpango na Lingard, kwa kuwa wameshindwa kumtumia kwa mechi nyingi huenda wanataka kupata chochote zaidi.United wanaamini bado wanaweza kumtumia
Ole Gunnar amesema kuwa staa huyu alilazimika kujitenga katika mazoezi ya peke yake mara kadhaa kwa sababu ya Corona. Na amesisitiza kuwa anafanya jitihada katika mazoezi.
“Anafanya jitihada kwenye mazoezi. Kwa bahati mbaya amelazimika kujitenga mara kadhaa, kwa sababu ya kupata, au kukaribia kupata au kuwa karibu na waathirika hata kama hakuwa nayo yeye” – Ole Gunnar.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?



Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri sana
felister
kila la kheri
warda
Sio mbaya Lingard anajua kiasi chake
Janeflora malisa
Safi
Magdalena
Habari njema kwa mashabiki
Sarah
Habari nzuri
Adelta
Ni vizuri kwa mashabiki
Angelina
Kila kheri
Sania
Jesse yupo vizuri
Rahmal
Vizuli
Hopemwaikuka
Inapendeza
Dorophina
Habari njema kwa mashabiki wa man u
Issa
Lingard ni moto sana
Gabriel
Safi sana