Manchester City Wamebamizwa Tena

Huu ni mwaka wa shetani kwa klabu ya Manchester City na kocha Pep Guardiola kwani leo tena mbele ya klabu ya Liverpool wamekubali kichapo cha mabao mawili kwa bila katika dimba la Anfield.

Manchester City leo wamefikisha mchezo wa saba bila kupata alama tatu huku katika michezo hiyo wakipoteza michezo sita na kupata sare mchezo mmoja, Hiki ikiwa rekodi mbovu zaidi kwa klabu hiyo na kwa kocha Pep Guardiola ambaye amekua na rekodi bora sana tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2016.manchester cityLiverpool wakiwa nyumbani walionekana wanahitaji kuendeleza kile ambacho wamekua wakikifanya msimu huu kwa ubora mkubwa, Kwani walianza kwa kasi wakiliandama lango la Man City na mapema dakika ya 12 tu Coady Gapko aliipatia bao la kuongoza Liverpool akipokea pasi nzuri ya Mohamed Salah na kuwapa uongozi majogoo wa Anfield.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Liverpool kuongoza kwa bao moja kwa bila lakini pia walionekana kutawala zaidi mchezo wakitengeneza nafasi nyingi za mabao lakini walishindwa kuweka mpira wavuni kutokana na nafasi hizo ambazo walizitengeneza huku Manchester City wao wakionekana kukosa maarifa kabisa mbele ya lango.Kipindi cha pili Liverpool walionekana kuendelea kutawala mchezo na kutengeneza nafasi za mabao huku ugonjwa wa kipindi cha kwanza ukiendelea kushindwa kuzitumia nafasi mpaka pale dakika ya 77 Luis Diaz kuchezewa madhambi kwenye eneo la hatari na Mohamed kufunga bao dakika ya 78 ya mchezo na kufanya ubao kusomeka mabao mawili kwa bila.

Liverpool wanaendelea kujisimika kileleni baada ya ushindi wa mabao mawili kwa bila leo wakifikisha alama 34 huku wakifuatiwa na Arsenal wenye alama 25 hivo wapo kileleni kwa alama 9, Wakicheza michezo 13 wakishinda 11 wakifungwa mchezo mmoja na kusuluhu mchezo mmoja pekee.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.