Manuel Locatelli Akutwa na Covid Baada ya Gemu na Villarreal

Kiungo wa kati wa Juventus na Italia Manuel Locatelli amepimwa na kukutwa na Covid-19, kwa mujibu wa ripoti ya Football Italia.

Nyota huyu alitakiwa kuitwa kuichezea nchi yake michuano ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Ureno mwezi huu lakini sasa anaonekana kuelekea kuikosa nafasi.

Manuel Locatelli
Manuel Locatelli

Locatelli alicheza kwa dakika 82 wakati Villarreal wakiichapa Juventus 3-0 na kuwaondoa kwenye Ligi ya Mabingwa, ikiwa ni jumla ya mabao 4-1 ukihusisha na sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza. Gerard Moreno, Pau Torres na Arnaut Danjuma walifunga mabao hayo.

Kwa kuzingatia kwamba Locatelli alikutana na wachezaji wa Villarreal kwa nyatati nyingi kwenye mechi, klabu hiyo ya Uhispania italazimika kufanya vipimo kadhaa na kufuata tahadhari zinazohitajika.

Kushinda kwa Villarreal kunamaanisha kwamba wako kwenye droo ya kesho ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa. Wamejiunga na vilabu vingine viwili vya Uhispania, Atletico Madrid na Real Madrid, pamoja na Benfica, Chelsea, Manchester City, Bayern Munich na Liverpool.


SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI

Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.

liverpool, Liverpool Kila Mtu Ashinde Mechi Zake., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe