Lautaro Martinez anaendelea kuwaumiza vichwa viongozi na mashabiki wa Inter Millan kutokana na kauli yake, “ninafuraha Inter lakini sijajua nini kitatokea kesho” hii ni kauli inayotahadharisha uwepo wake Inter kwa muda mrefu.
Martinez amehusishwa na usajili mkubwa wa kujiunga na miamba ya LaLiga – Barcelona na dirisha la usajili lilimalizika pengine tungeona hilo likitokea lakini haikuwa hivyo.
Akiwa na umri wa miaka 23 pekee, mpaka sasa katika michezo 5 ya Serie A ameshafunga magoli 3 na hakupendezwa na kitendo cha kutolewa katika kipindi cha pili kwenye mchezo dhidi ya Genoa.
Akizungumza kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Shakhtar Donetsk, Martinez amesema, “Ninafanya kazi kubwa kila siku kujiimarisha zaidi. Ninataka kujitoa kikamilifu kwa Inter na wachezaji wenzangu.
“Ninafuraha kuwa Inter. Tunajitahidi kufanya kila tuliwezalo ili tupate mataji na kuirudisha Inter inapotakiwa kuwa.
“Hiki ndicho ninachokiwaza leo. Sijui kitakacho tokea kesho lakini leo ninapenda kuwaambia kuwa ninafuraha kuwa Inter.
“Ninawashukuru mashabiki kwa upendo wanaonionesha na pia kwa wafanyakazi wote wa Inter. Hili ndio jambo muhimu kwangu.”
Inter hawajawahi kupoteza mchezo dhidi ya timu za Ukraine na mchezo wao wa mwisho dhidi ya Shakhtar Donetsk, Inter walishinda 5-0 katika nusu fainali ya Europa msimu uliopita.
Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.



Dorophina
Uongozi hautokubari haondoke inter mda ukifika
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri martinez
aisha
Martinez usiondoke jamani mashabiki wa inter tumekuzoea
Sabrina
Martinez bado inter inakuhitaji
Povel
Hapo martizen Kama Barcelona Kama watapeleka ofa kubwa ya kushawish uongozi na martinez mshahara wakutosha natumain wanawez kumuuza martinez lautaro hapo kazi kwa Barcelona kupelek dau la kuelew kwa kinda huyo
Hopemwaikuka
Dah
Issa
Martinez ana mshawasha na barca kwakua yupo mchezaj anaemuhsudu mess ambae yupo nae argentina
Sauda
Baki hapo hapo panakufaa.
Fatina mfingi
Kambi popote kikubwa masai tyu
Mwajumah
Vizuri sana martizen
Tatu
Martizen bado inter wanakuitaji
Elika
Abakie hapo mbona panamfaa sana
warda
Bora asepe tu
Ernest
Deal kubwa lipo mbele yake hii ipo wazi lazima atachangamkia fursa ya Barca