Coman Aitamani Treble Tena na Mashabiki Uwanjani.

Kingsley Coman anataka Bayern Munich kushinda tena mataji matatu (treble) ndani ya msimu mmoja kama walivyofanya msimu uliyopita lakini safari hii anatamani mashabiki kuwepo watakapo pata mafanikio hayo.

Maambukizi ya virusi vya Corona yalisababisha mashabiki ulimwenguni kote kutohudhuria katika viwanja vya michezo mara baada ya soka kurejea, wakati Bayern Munich walifanikiwa kushinda mataji matatu Bundesliga, DFB-Pokal na Champions League bila uwepo wa mashabiki.

Coman alifunga goli pekee na la ushindi katika fainali ya Champions League dhidi ya Paris Saint-Germain mwezi Agosti na kufanya miamba hiyo ya Bavaria kuwa timu ya kwanza katika historia ya mashindano hayo kushinda taji kwa kushinda mechi zote.

Coman Aitamani Treble Tena na Mashabiki Uwanjani.
Wachezaji wa Bayern Munich

Bayern waliendeleza rekodi yao ya ushindi kwa kuifunga Atletico Madrid 4-0 katika kundi A kwa mchezo wa ufunguzi, na mchezo ujao ni dhidi ya Lokomotiv Moscow siku ya Jumanne.

Mashabiki wameruhusiwa kuhudhuria viwanjani nchini Ujerumani msimu huu na Coman anatumaini watashuhudia Bayern ikinyanyua mataji matatu tena msimu 2020-21.

“Yah ni kweli tunataka tushinde treble kila mwaka, tumefanya hivyo msimu uliyopita, bahati mbaya ilikuwa bila mashabiki,” Coman aliiambia CBS Sports.

“Huenda wakaruhusiwa tena mwaka ujao tunataka kufanya kama tulivyofanya tena mbele ya mashabiki zetu.

Coman alifunga mara mbili kwenye mechi dhidi ya Atletico Madrid na kuchangia kuuanza msimu mpya wa Champions League kwa ushindi.


Tsh.160,000,000 Kushindaniwa!

Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.

Kamata Mkwanja wako HAPA🤑

15 Komentara

    Coman anachosema yuko sahihi kabisa

    Jibu

    Duuh hatari sana Coman ameliona hilo

    Jibu

    Coman kingsley yupo sahihi lakin kipind hch cha janga la corona ni vigumu sana kuona mashabik wakiingiah uwanjan ila tuwape muda janga liondoke ili hali irud Kama mwanzo iliwawez kurud mashabik viwanjan

    Jibu

    Coman yuko vzur kinyama

    Jibu

    Kwa moto alionao huyu treble kwa mara ingine

    Jibu

    Coman anakiu ya ushindi mbele ya mashabiki lakini ndo haiwezekani kwa kipindi hiki cha corona

    Jibu

    Mashabiki hawatoweza kuhudhuria uwanjani kipindi cha Corona

    Jibu

    Duuh corona inatisha sanaa

    Jibu

    Coman yupo vizuri sana

    Jibu

    Coman yupo sahii

    Jibu

    Coman yupo vizuri

    Jibu

    vigumu sana kuona mashabik wakiingiah uwanjan ila tuwape muda janga liondoke ili hali irudi Kama mwanzo iliwawez kurud mashabik viwanjani

    Jibu

    Yuko sahihi kwa kile alichokisema

    Jibu

    Kila kitu mipango tu

    Jibu

    Bayern wanaweza kupata changamoto kubwa sana kutoka kwa timu nyingine lakini bado wananafasi ya kufanya makubwa tena

    Jibu

Acha ujumbe