Juventus Yasubiri Majibu ya COVID-19 kwa Ronaldo

Klabu ya Juventus inasubiri majibu baada ya vipimo kwa mshambuliaji Christiano Ronaldo kuangalia kama anaweza kucheza dhidi ya Barcelona katika mashindano ya Champions League.

Ronaldo amewekwa katika matazamio tangu ajulikane kuwa na maambukizi ya COVID-19 wakati wa michezo ya kimataifa akiwa na timu yake ya Portugal mwezi huu, na ameikosa michezo kadhaa dhidi ya Crotone na Hellas Verona katika Serie A pia alikosa mchezo wa UEFA dhidi ya Dynamo Kiev.

Maamuzi kuhusu kupatikana katika mchezo ujao wa Champions League dhidi ya Barcelona ambako kuna mpinzani wake wa muda mrefu Lionel Messisiku ya Jumatano yatatolewa hivi karibuni.

“Amefanya vipimo siku ya leo Jumanne kama watu wote, tunapaswa kusubiri majibu ya vipimo, nadhani yataletwa jioni,” kocha wa Juve Andrea Pirlo alisema.

“Tunatakiwa tusubiri majibu kisha tutaangalia kama atacheza kila kitu bado hakijulikani tuna tumaini tutamuangalia kama atakuwa vizuri kwaajili ya mchezo.

Pirlo pia alizungumzia kuhusu eneo la ulinzi ambalo lina watu kama Giorgio Chiellini na Matthijs de Ligt hawatokuwepo na Leonardo Bonucci ambaye anakabiliwa na kutokuwa fit.

“Kesho tutaangalia wachezaji gani watakao weza kucheza Barcelona ni timu imara tutatakiwa kucheza mchezo mzuri.

“Wachezaji watatakiwa kujitoa sana wenyewe na kucheza kwa bidii.Weston McKennie anafanya mazoezi lakini sidhani kama ataweza kucheza eneo la ulinzi dhidi ya Barcelona.


Tsh.160,000,000 Kushindaniwa!

Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.

Kamata Mkwanja wako HAPA🤑

12 Komentara

    Covid 19 ni tatizo kubwa inapaswa vilabu vichukue tahadhari kuepuka maambukizi zaid

    Jibu

    Mungu atamjalia atakua salama

    Jibu

    Hapo naona juventus wanajaribu Kama kulazimisha cr7 kucheza kwny mchezo huo muhimu lakin mm naona juventus wangejaribu kumuweka cr7 penden hatakama hatakuwa na negative covid 19 ilikumpa muda wa kupumzika zaid na kufany mazoez kulik kuforce kucheza kwny mtanange wababe kutok catalunya asubir tu

    Jibu

    Mungu amsaidie awepo kwenye mechi dhidi ya barca maana yeye ndio msaada mkubwa pale juve

    Jibu

    Duuh corona ni tatizo sana ila atapona pia atarejea kazini kwake

    Jibu

    Corona ishindwe kwa Ronaldo..

    Jibu

    Corona sio powah

    Jibu

    Daaah corona hii ni tishio sana

    Jibu

    Duu sio poa gonjwa atari Sana hili

    Jibu

    Corona imehalibu mipango yake Ronald

    Jibu

    Mungu amsaidie apone huu ugonjwa sio poa

    Jibu

    Jamani CR7 Nae kapata huu ugojwa sio poa

    Jibu

Acha ujumbe