Mbappe Akana Taarifa Za Yeye Kutaka Kuondoka Psg

Mchezaji wa Psg Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 23 na raia wa Ufaransa  ameweka wazi kuwa ripoti iliyokuwa ikisambaa kuwa anataka kuondoka klabuni hapo Januari sio za kweli.

 

Mbappe Akana Taarifa Za Yeye Kutaka Kuondoka Psg

Mbappe, ambaye alicheza katika mechi ya hapo jana walipokuwa nyumbani kumkaribisha Marseille na kushinda kwa bao 1-0 ilisemekana kuwa alihisi kuwa amesalitiwa na Psg kutokana na kuvunja masharti waliyokuwa wamewekeana wakati anasaini mkataba mpya wa kumbakisha klabuni hapo.

Mchezaji huyo aliyeshinda Kombe la Dunia mwaka 2018, alitia saini kandarasi mpya mwezi Mei, baada ya miezi kadhaa ya mashaka, lakini aliripotiwa kutokuwa na utulivu kwa mara nyingine baada ya kushindwa kutimiza matakwa yake kwa mbinu na kuajiriwa.

Mshauri wa kandanda wa PSG Luis Campos alikanusha kwa msisitizo taarifa hizo kwa kudai Mbappe hajafahamisha klabu hiyo kuhusu nia yake ya kuondoka klabuni hapo huku kocha mkuu Galtier pia akieleza kuchanganyikiwa juu ya uvumi huo.

Mbappe Akana Taarifa Za Yeye Kutaka Kuondoka Psg

Kutokana na uvumi huo kuwa mkubwa zaidi Mbappe ametoa maoni yake kuhusu ripoti hizo, ambazo ziliibuka muda mfupi kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa ya PSG dhidi ya Benfica siku ya Jumanne, na anasisitiza kuwa si za kweli na akasema kuwa;

“Nina furaha sana, sikuwahi kuomba kuondoka Januari,” alisema, akizungumza na vyombo vya habari vya Ufaransa. “Taarifa zilitoka siku ya mechi, sikuelewa, sijahusika hata kidogo na habari hii, nilishtuka kama kila mtu.

Mbappe alikanusha madai hayo huku akiongeza kwa kusema kuwa watu wanadhani kuwa anahusika, lakini hahusiki kabisa na watu wakaribu naye walishangaa uvumi huo pia ndipo baadae wakalazimika kukabiliana nayo na kusema ukweli ana furaha sana klabuni hapo.

Mbappe Akana Taarifa Za Yeye Kutaka Kuondoka Psg

Mchezaji huyo alikuwa akilengwa na Real Madrid kabla ya kukubali kuongeza muda wa kukaa Psg. Alisisitiza kuwa yeye ni mchezaji wa mpira wa miguu na jambo muhimu kwake ni kucheza, kujituma, kwa uwezo wake wote uwanjani na sasa wanalenga mataji.

Mbappe ameanza msimu huu akiwa na kiwango kizuri mbele ya lango, akifunga mabao 12 katika michezo 14 katika michuano yote akiwa na mabingwa hao wa Ufaransa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.