Mbappe Anazidi Kuwapa Matumaini Real Madrid

Real Madrid wanaripotiwa kushawishika kuwa watashinda mbio za kuwania saini ya Kylian Mbappe hapo 2022.

Mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain anatazamiwa kuwa mchezaji huru mwishoni mwa kampeni ya sasa, huku mazungumzo ya kurefushwa makataba wake yakiendelea kugonga mwamba.

Real Madrid ilishuhudia ofa yao ya pesa ndefu ikikataliwa na PSG wakati wa mechi za mwisho za msimu wa joto, na wanapendekezwa kuwa kwenye nafasi nzuri ya kumpata Mbappe kwa uhamisho wa bure 2022.

Mkataba wa Kylian Mbappe Uliandaliwa Mara 7 Madrid!
Kylian Mbappe

Kwa mujibu wa AS, Real Madrid wana ‘uhakika’ kwamba staa huyu atavaa jezi ya Real Madrid msimu wa 2022-23 na kuendelea, huku mshindi huyo wa Kombe la Dunia akiwa hana nia ya kuongeza mkataba wake wa PSG.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa Mbappe anajihisi kama ni msaidizi tu PSG akiwa pembeni ya Neymar na Lionel Messi, na angefurahi kuwa chachu ya mabadiliko kule Real Madrid.

Hadi sasa amefunga mabao tisa na kusaidia mengine 12 katika michezo 20 ya michuano yote msimu huu, ikijumuisha asisti 14 kwenye mechi 15 za Ligue 1.


MUDA WA KUJIACHIA NA CARNAVAL JACKPOT

Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.